Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

watoto wa chini ya miaka 18 ni asilimia 50 ya watu wanaoishi kwenye nchi zenye mizozo:UN

Watoto waliokuwa wakitumikishwa vitani wasimulia madhila yaliyowakumba kwa balozi wa Sweden kwenye Umoja wa Mataifa Olof Skoog wakiwa ziarani ya baraza la usalama kama kwa ajili ya watoto kwenye mizozo.
UN Photo/Isaac Billy
Watoto waliokuwa wakitumikishwa vitani wasimulia madhila yaliyowakumba kwa balozi wa Sweden kwenye Umoja wa Mataifa Olof Skoog wakiwa ziarani ya baraza la usalama kama kwa ajili ya watoto kwenye mizozo.

watoto wa chini ya miaka 18 ni asilimia 50 ya watu wanaoishi kwenye nchi zenye mizozo:UN

Amani na Usalama

Ingawa watoto hawana jukumu kubwa katika vita, mamilioni miongoni mwao wanajikuta katikati ya machafuko ambayo sio watazamaji bali walengwa, umesema Umoja wa Mataifa ukizinfdua muongozo wa kuwalinda watoto katika hali za vita.

Katika uzinduzi huo uliofanyika leo  siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya watoto kama askari kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichojikita na ujumuishwaji wa ulinzi wa watoto katika michakato ya amani , Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres amesema watoto wapatao milioni 250 wanaishi katika nchi zilizoathirika na migogoro.

Ameongeza kuwa watoto wa umri wa chini ya miaka 18  ni zaidi ya asilimia 50 ya watu wote walioko katika nchi zilizoathirika na vita, wako katika hatari na hawawezi kujilinda na athari za vita hivyo.

“Mwaka 2018 zaidi ya watoto 12,000 waliuawa au kujeruhiwa katika vita ikiwa ni idadi kubwa Zaidi kurekkodiwa tangu mwaka 1996 wakati Baraza Kuu lilipoanzia jukumu la mwakilishi maalum kuhusu watoto na mizozo ya silaha. Visa hivyo viliorodheshwa na kuthibitisha Zaidi ya matukio 24,000 ya ukiukwaji iikilinganishwa na 21,000 mwaka 2017.” Amesema Bwana Guterres.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
UN /Manuel Elias
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Katibu mkuu amekumbusha kwamba mashambulizi kwenye shule na hospitali yanayotokana na vita yanawanyima watoto haki yao ya kupata elimu na huduma za afya na yanazilazimisha familia kuzikimbia nyumba zao. zaidi yah apo amesema watoto wanaweza kuwa waathirika wa ukatili ukiwemo wa kingono na utekwaji.

Wanaweza kufundishwa kutumia silaha za mauaji, au kutumikishwa kama wapishi na matarishi. Ukiukwaji huu husababisha athari za muda mrefu kwa watoto na jamii zao. Athari hizo zinaweza kuwa chachu ya madchungu na chuki ambayo husababisha itikadi kali, na kuanzisha mzunguko wa mvutano na machafuko.”

Kikao hicho cha Baraza la Usalama kimeendeshwa na waziri wa mambo ya nje wa Ubelgiji Philippe Goffin na kimehudhuriwa na mfalme Felipe wa nchi hiyo.

Na wakati wa kikao hicho Katibu Mkuu Antonio Guterres ametangaza kuzindua “muongozo kwa ajili ya wapatanishi kuhusu ulinzi wa watoto katika hali za vita vya silaha.”

Na wakati wa kikao hicho Katibu Mkuu Antonio Guterres ametangaza kuzindua “muongozo kwa ajili ya wapatanishi kuhusu ulinzi wa watoto katika hali za vita vya silaha.”

Watoto katika jimbo la Wardak afghanistan
UNAMA/Fardin Waezi
Watoto katika jimbo la Wardak afghanistan

Mkakati Madhubuti

Katibu Mkuu amezungumzia hatua zilizopigwa katika kuelimisha umma kuhusu ukiukwaji, akipongeza sehemu ya mkakati wa Umoja wa Mataifa wa ufuatiliaji na utoaji taarifa ulioanzishwa mwaka 2005 ambako kwa muda umekuwa na uwezo wa kubadili tabia, kuzuia ukiukwaji mkubwa na kuwalinda watoto.

Amezungumzia kazi inayofanywa na mwakilishi wake maalum kuhusu watoto kwenye migogoro ya silaha na kampeni ambazo zimesaidia kulketa muafaka wa kimataifa kwamba “watoto asilani wasitumike katika mizozo” huku akikiri kwamba pamoja na juhudi zote hizo “idadi ya visa vya ukiukwaji mkubwa wa haki dhidi ya watoto  kwenye mogogoro vinaendelea kuongezeka.Sote tunapaswa kufanya juhudi zaidi “amehimiza.

Muongozo mpya kwa ulinzi wa watoto

Kama hatua inayofuata ya kuwaweka watoto katika kitovu cha ulinzi, ujenzi wa mani na juhudi za kuzuia migogoro , Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuzinduliwa kwa muongozo mpya ambao unaweka mbele maslahi ya watoto na haki zao katika wakati wote wa vita, kuanzia juhudo za kuzuia  hadi upatanishi na kujijenga upya , kupitia maendeleo jumuishi na endelevu.

Muongozo huo unatoa uwezo wa kuendesha tathimini mgogoro kwa ajili ya wapatanishi na washauri.

“Kwa kujumisha hatua maalum katika kulinda watoto kwenye michakato ya amani tunaweza kufikia matokeo yanayoonekana kwa ajili ya watoto na amani.

Pia amesema tukizichagiza nchi zote wanachama , mashirika ya kikanda na kieneo, waopatanishi na wengine wanaohusika na mchakato wa amani kutumia kikamilifu muongozo huu, hiyo pekee haitoshi” amesema Guterres .

Mabegi ya shule ya watoto yakiwa yametandazwa kama mfano wa makaburi kwenye viwanja vya makao makuu ya UN jijini New York, Marekani kuashiria watoto waliokufa kwenye maeneo ya mizozo mwaka 2018.
UN News/Elizabeth Scaffidi
Mabegi ya shule ya watoto yakiwa yametandazwa kama mfano wa makaburi kwenye viwanja vya makao makuu ya UN jijini New York, Marekani kuashiria watoto waliokufa kwenye maeneo ya mizozo mwaka 2018.

Makaburi yenye ndoto

Katibu Mkuu amehitimisha kwa kukumbusha maonesho ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF yam waka 2018 ambapo eneo la uwanja wa umoja wa Mataifa la upande wa Kaskazini mjini New York Marekani liliwekwa mifuko ya watoto wa shule ya kubebea vitabu jumla 3,758 mithili ya makaburi ambapo kila mmoja ulikuwa unawakilisha mtoto mmoja aliyeuawa mwaka huo kwenye vita. “Kusimama kwenye makaburi haya yliyojaa ndoto iliniumiza sana. Ni wajibu wetu kimsingi kama viongozi kufanya kila tuwezalo kwa uwezo wetu kuwalinda watoto, mustakabali wetu dhidi ya ghasia na madhila ya vita ambavyo haviwahusu kabisa” amesema Katibu Mkuu

Msisitizo wa ahadi

Wakati wa kikao hicho cha Jumatano Baraza la Usalama lilitoa tarifa ya raia wake ambayo miongoni mwa mambo mengine imerejea kusisitiza kwamba “ulinzi wa watoto katika maeneo yenye mizozo ya silaha ni lazima iwe kipengele muhimu cha mkakati wowote wa kutatua mizozo na kudumisha amani.”

Pila imesisitiza kwamba umuhimu wa kuchukua mkakati mpana wa kuzuia migogoro ambao utashughulikia kwa kina mizizi ya vita vya silaha ili kuimarisha ulinzi kwa watoto katika misingi ya muda mrefu.

Mtoto ripota wa RTBF  Héloïse Lejeune akimuhoji Katibu Mkuu antonio Guterres kandoni mwa mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu ulinzi wa watoto katika mizozo ya silaha.
Belgium Ministry of Foreign Affairs
Mtoto ripota wa RTBF Héloïse Lejeune akimuhoji Katibu Mkuu antonio Guterres kandoni mwa mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu ulinzi wa watoto katika mizozo ya silaha.

watoto wawe kitovu cha juhudi zetu

Kwa upande wake Smail Chergui kamishina wa amani na usalama wa Muungano wa afrika AU, amesema “watoto lazima wake kitovu cha juhudi zetu zote za kuzuia migogoro na kuitatua. Akizungumza kwa njia ya video kwenye mkutano huo ameongeza kuwa “kuna haja ya hatua Madhubuti za kuepuka na kukabiliana na mifumo yote ya ukatili, utelekezaji na unyanyasaji wa watoto.”

Amesisitiza kuwa wakati wa majadiliano yoyote ya amani maskahi ya watoto lazima yawe kipaumbele cha kwanza na kwamba ukiukwaji wa haki za watoto sio tu lazima uzuiliwe lakini pia lazima ushughulikiwe kabla, wakati na baada ya vita.

Ameonya kwamba “Kutoshughulikia ukiukwaji wa haki za watoto kunazalisha hulka ya ukwepaji sheria , kutokuwepo haki na kutofuata sheria ambako kunaweza kuwa ndio chachu ya vita na pia kutoa mazingira ya kurejea tena katika machafuko.”

Kwa kuzingatia athari mbaya zinazosababishwa na vita kwa watoto na husuasani kukiukwa kwa haki zao za msingi za binadamu  na uhuru, kamishina huyo wa Muungano wa afrika amesema ni muhimu kwamba “wadau wote wanaohusika katika upatanishi na mchakato wa amani , wajumuishe lugha ya ulinzi wa watoto na vifungu katika mikataba ya amani