Sayansi ni somo shirikishi, hebu tuwashirikishe wanawake na wasichana:Guterres

11 Februari 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ingawa sayansi ni somo shirikishi lakini bado sayansi hiyo inabakizwa nyuma na pengo la kijinsia

Guterres ameyasema hayo katika ujumbe wake maalum kuhusu siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi ambayo kila mwaka huadhimishwa Februari 11. Akisistiza umuhimu wa ujumuishaji wanawake na wasicha katika somo jilo Guterres amesema

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES )

“Wasichana na wavulana wote hufanya vyema katika sayansi na hisababi lakini ni sehemu ndogo tu ya wanafunzi wa kike katika elimu ya juu ndio wanaochagua kusoma sayansi. Ili kukabilina na changamoto za karne ya 21tunahitaji kutumia uwezo wetu wote na hilo linahitaji kuvunja matabaka yote ya kijinsia “

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa hii inaamanisha kusaidia kazi za wanasayansi wanawake na watafiti na kwamba misingi ya uwezeshaji wanawake iliyoanzishwa na UN Women inatoa muongozo kwa makampuni na wengine.

Ameongeza kuwa

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES )

“Katika mwaka huu ambao tunaadhimisha miaka 25 ya azimio la Beijing na jukwaa la kuchukua hatua hebu tulete uharaka mpya wa kuchagiza fursa za wanawake na wasichana katika elimu ya sayansi, mafunzo na ajira.”

Ametaka katika siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi dunia itoe ahadi ya kuziba pengo la uswa wa kijinsia katika sayansi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter