Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na harakati za kuchagiza malezi bora kwa watoto wa mitaani Kenya

UNICEF imesema Novemba 2018 kuwa watoto wawili kati ya watatu wanahitaji msaada wa kibindamu.
UNICEF/Ashley Gilbertson
UNICEF imesema Novemba 2018 kuwa watoto wawili kati ya watatu wanahitaji msaada wa kibindamu.

UNICEF na harakati za kuchagiza malezi bora kwa watoto wa mitaani Kenya

Haki za binadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kenya limetoa wito kwa watoto wa mitaani kujumuishwa katika jamii pale panapowezekana

iwe ni kwa kupitia ndugu au walezi kama sehemu ya kampeni ya juhudi za kutoa uelewa wa faida za malezi kwenye familia.

Kutana na kijana Samora Asere yeye ni mpiga picha na mmoja wa watu ambao katika utoto wake aliishi katika taasisi ya kulelea watoto baada ya kujipata mitaani.

Anasema baadaye alijumuika na familia yake lakini akiwa na umri mkubwa.

Kijana Asere anasema kwamba alikimbia nyumbani kufuatia mazingira yaliyokuwepo na kwamba.

(Sauti ya Asere)

UNICEF inasisitiza umuhimu wa malezi katika mazingira yanayofaa kwa ajili ya kulinda watoto dhidi ya unyanyasaji na mateso na inashirikiana na serikali kujenga mikakati na programu zinazochagiza malezi kutoka kwa wanafamilia kwa mtoto.

Kijana Mark mwenye umri wa miaka 14 ni mmoja wa watoto waliokimbia hapa akielezea kilichomsukuma kufanya hivyo.

(Sauti ya Mark)

Kwa Mark ameunganishwa na familia yake, Sarah ni mamake mzazi

(Sauti ya Sarah)

“Kwa hakika Mark ni kijana barubaru na hatukujua, hakufahamu alichokuwa anawaza kwani tulijua bado mdogo na siku hizo tunasema naye na amebadilika amekuwa kijana mzuri na anaweza kufanya chochote hatuna hofu hata wakati ambao hatupo nyumbani.”

(Play Nats)

Ili kuhakikisha kwamba Mark anasalia nyumbani na kuondoa mawazo ya kukimbia mamake anamhakikishia upendo wake ambao Mark anaupokea na kuahidi kutowatia aibu wazazi wake.