Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ISIL bado ni kitovu cha tishio la ugaidi :UN

Sinjar nchini Iraqi Kurdistan ilivamiwa na wapiganaji wa ISIL wakati kundi lenyewe la kigaidi lilidhibiti mji.
UN OCHA/GILES CLARKE
Sinjar nchini Iraqi Kurdistan ilivamiwa na wapiganaji wa ISIL wakati kundi lenyewe la kigaidi lilidhibiti mji.

ISIL bado ni kitovu cha tishio la ugaidi :UN

Amani na Usalama

Licha ya kupoteza udhibiti wa moja ya maeneo ya mwisho waliyokuwa wakiyahidhi nchini Iraq na kuuawa kwa kiongozi wake, kundi la kigaidi la ISIL linasalia kuwa kitovu cha tishio la ugaidi kimataifa amesema afisa wa Umoja wa Mataifa kwenye Baraza la usalama hii leo Ijumaa.

Akiwasilisha ripoti ya karibuni ya Umoja wa Mataifa kuhusu ISIL Vladimir Voronkov, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi, ameitaka jumuiya ya kimataifa kusalia na mshikamano katika kupambana na kundi hilo ambalo limerefusha mbawa hadi Afrika, Ulaya na Asia.

“ISIL imeendelea kuibuka na kusambaa kimataifa mtandaoni nan je ya mtandao, likidhamiria kufufua uwezo wake katika operesheni ngumu za kimataifa. Wafuasi wa kikanda wa ISIL wanaendelea kusaka mikakati ya kujipenyeza kwenye maeneo ya vita kwa kuwatumia waathirika wa madhila.”

Ameongeza kuwa maelfu ya raia wa kigeni walisafiri kwenda Syria na Iraq kuunga mkono ISIL kundi ambalo hujulikana pia kama Daesh, na inakadiriwa kwamba takriban 27,000 bado wako hai na wataendelea kutoa vitisho vya muda mfupi na muda mrefu.

Bwana Voronkov amesema kwa mfano nchi za Ulaya hofu yao ni kuhusu kutarajiwa kuachiliwa kwa takriban wahukumiwa 1000 wa ugaidi ambapo baadhi yao ni wapiganaji wa zamani.

Vladimir Voronkov, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Ugaidi, ajulisha mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu vitisho vya amani na usalama wa kimataifa unaosababishwa na vitendo vya kigaidi.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Vladimir Voronkov, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Ugaidi, ajulisha mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu vitisho vya amani na usalama wa kimataifa unaosababishwa na vitendo vya kigaidi.

 

“ISIL ilipoteza eneo lake la mwisho ililokuwa ikilidhibiti nchini Syria Machi mwaka jana na limeshuhudia mabadiliko ya uongozi baada ya kifo cha Al-Baghdad mwezi Oktoka mwaka jana , lakini ripoti hii inaonyesha kwamba kundi hilo linasalia kuwa kitovu cha tishio la ugaidi wa kimataifa. Ni lazima tuwe makini na tuungane katika kukabiliana na jinamizi hili.”

Baraza pia limesikia kutoka kwa Mona Freij mwakilishi wa asas iza kiraia ambaye alikimbia kutika mji wa Raqqa Syria baada ya wapiganaji wa ISIL waliojiahami na silaha za kila aina walipovamia nyumba yake mweszi Septemba mwaka 2014.

Alifanikiwa kutoroka baada ya jirani yake kuwapotosha wapiganaji hao kuhusu mahali aliko lakini watu wwengine wa familia yake walikamatwa , kuteswa na kuajwa na majeraha ya kisaikolojia.

Bi. Freij alirejea Raqqa mwaka 2017 baada ya uasi na jinamizi la daesh kumalizika. “Wanawake walinyimwa elimu na walikuwa katika hali ngumu sana. Nilikutana na watoto yatima na wakanieleza walilazimishwa kujiunga na daesh na wanawake walilazimishwa kuzaa na wapiganaji wa Daesh na endapo walikataa matakwanza ya kingono ya wapiganaji hao waliadhibiwa vikali. Walishindwa kujizuia kupata mimba, walikuwa mateka ambao walilazimika kukidhi matakwa ya mashetani. Kila siku wanakabiliwa na mtihani mgumu wa kutambua ni nani baba wa watoto wao.”

Bwana Voronkov ameliambia Baraza la Usalama kwas asa hofu kubwa ni watu zaidi ya 100,000 wanaohusiana na ISIL wengi wakiwa ni wanawake na watoto walioko katika vizuizi na makambi ya wakimbizi wa ndani.