Pamoja na mlipuko wa virusi vya corona China, waathirika wa VVU wataendelea kuangaliwa vizuri-UNAIDS

6 Februari 2020

Shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI, UNAIDS limesema linafanya kazi kwa ukaribu kwa kushirikiana na mamalaka nchini China kuhakikisha pamoja na uwepo wa virusi vya corona, huduma kwa wagonjwa wa Virusi Vya ukimwi, VVU wanaendelea kupata huduma.

Kwa kuanzia UNAIDS imeetuma salamu zake za rambirambi kwa familia amzao wamepoteza wapendwa wao kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, 2019-nCoV.

Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Winnie Byanyima amesema, “China imefanya juhudi kubwa kuudhibiti mlipuko hu una nina imani na uwezo wa China kudhibiti janga hilo. Katika wakati huu mgumu, UNAIDS inatoa msaada wake kwa juhudi za kimataifa za kuzuia kuenea kwa virusi.”

Taarifa ya UNAIDS iliyotolewa Alhamis hii mjini Geneva Uswisi, imesema katika maeneo ambayo yameathiriwa na mlipuko wa virusi vya corona, harakati za kutoka eneo moja kwenda jingine zinaweza kubanwa au kupunguzwa zikiwemo za kwenda hospitali kupata huduma kwani hivi sasa hospitali zinashughulika zaidi nan a ongezeko la wagonjwa wa virusi vya corona.

UNAIDS imepongeza kituo cha kitaifa cha China kinachohusika na UKIMWI na magonjwa ya zinaa kwa kuchukua hatua za haraka  kuhakikisha watu wanaoishi na VVU na ambao wako mbali na nyumbani kwao katijka kipindi hiki cha mlipuko na kufungwa kwa makazi, wanapata matibabu yao ya kila mwezi zikiwemo kupata dawa za kufubaza virusi.

UNAIDS imesema haina uhakika bado na idadi ya watu ambao wanaishi na VVU na wameathirika na virusi vya corona huko nchini China, lakini inaendelea kufuatilia maendeleo ya tatizo hilo.

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter