Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Janga la njaa lanyemelea Sudan Kusini WFP yatiwa hofu kubwa

Usambazaji wa chakula mjini Beira, Msumbiji. Katika shule iliyogeuzwa kuwa makazi, familia 70 zikipokea chakula kutoka WFP. Familia nyingi zimeathirika kutokana na kimbunga.
WFP/Deborah Nguyen
Usambazaji wa chakula mjini Beira, Msumbiji. Katika shule iliyogeuzwa kuwa makazi, familia 70 zikipokea chakula kutoka WFP. Familia nyingi zimeathirika kutokana na kimbunga.

Janga la njaa lanyemelea Sudan Kusini WFP yatiwa hofu kubwa

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP linashtushwa na hofu mpya ya viwango vya janga la njaa wakati huu likikabiliwa na ukata wa fedha za msaada huko Sudani Kusini

Eneo la Al Sudd ni moja ya bwawa kubwa zaidi ulimwenguni, ukubwa wake ni sawa na nchi nzima ya Hispania. Maelfu ya watu wanaokimbia mapigano wamekimbilia kwenye eneo la bwawa hili na kwenye visiwa vidogo kama Nyal.

Debora Nyakueth mwenye umri wa miaka 28 alikimbia na watoto wake watano wakati mapigano yalipozuka kwenye mji wa Leer.

Kwa mwezi mzima Deborah na watoto wake walijificha katika bwawa hili wakihatarisha Maisha yao dhidi ya mashambulizi ya mamba na viboko, wakiishi kwa kula maua ya bwawani aina ya lili kabla hawajapata hifadhi kwenye kisiwa kidogo cha Nyal

(SAUTI YA DEBORAH NYAKUETH)

“Kinachotuathiri Zaidi ni njaa. Inawaumiza sana kina mama kuona watoto wao walio na njaa wanalia. Kunapokuwa na mgao wa chakula tunakuwa na chakula kwa ajili ya watoto na watoto wanaotabasamu kwa sababu wamekula inakufurahisha kama mama.”

WFP inatumia ndege kudondosha chakula kama suluhisho la mwisho kuwafikia watu waliojitenga kwenye maeneo kama Nyal. Kwa wakati huu WFP ina ndege tatu zinazoendesha operesheni za kudondosha chakula  Sudan Kusini.

Na ndege kubwa kabisa imejazwa tani 34 za chakula cha kutosha kuwalisha watu 3000 kwa mwezi mmoja.

watoto wenye uatpiamlo uliokithiri wanapimwa na kupatiwa matibabu. Athari za vita vilivyowafanya maelfu ya watu kufungasha virago na kuzikimbia nyumba zao vinatarajiwa kuongeza idadi ya visa vya utapiamlo katika katika miezi ijayo endapo msaada hautoongezeka.

Matthew Hollingworth ni mkurugenzi wa WFP Sudan Kusini

(SAUTI YA MATTHEW HOLLINGWORTH)

Tunajua tunahitaji kuwasaidia watu milioni 5.5 Sudan Kusini kwa msaada Fulani wa chakula. Lakini endapo hatutopata rasilimali za kutosha kuwafikia watu wote hao itabidi tufanye maamuzi magumu . Itabidi tujikite tu na wale ambao hawana kabisa uhakika wa chakula nchini humu , kuondoa njaam kuzuia baa la njaa linalonyemelea. Lakini hilo pia linamaanisha kwamba baadhi ya watu watakubwa na pengo kubwa, inamaanisha hatutoweza kumsaidia kila mtu.”

Debroha anasema suluhu pekee ni amani endapo tutakuwa na amani watoto wetu wataweza kwenda shule na wanaporejea nyumbani watakuta chakula ma hali hiyo itawafurahisha.