Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasichana wa Namibia wako tayari kubobea katika programu za Kompyuta

Kundi la wasichana wa Namibia ambao walishiriki katika kambi ya mafunzo ya programu za Kompyuta (AGCC) mjini Pretoria, Afrika Kusini.
UN Namibia
Kundi la wasichana wa Namibia ambao walishiriki katika kambi ya mafunzo ya programu za Kompyuta (AGCC) mjini Pretoria, Afrika Kusini.

Wasichana wa Namibia wako tayari kubobea katika programu za Kompyuta

Wanawake

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Namibia imewapatia wasichana sita kompyuta mpakato ili ziweze kuendeleza ujuzi wao wa programu za kompyuta.

Wasicaha hao ni wale ambao mnamo mwezi April mwaka jana wa 2019, walijiunga na wasichana wengine 39 kutoka Botswana, Eswatini, Lesotho, Afrika Kusini, Tanzania na Zimbabwe ili kushiriki katika kambi ya “Wasichana wa Afrika wanaweza kubobea katika programu za Kompyuta” yaani “African Girls Can Code,”, AGCC iliyofanyika mjini Pretoria nchini Afrika Kusini.

Programu ya AGCC inalenga kuwafikia wasichana 2000 kutoka kote barani Afrika wenye ujuzi wa dijitali, ikiwemo mifumo ya Kompyuta, programu za Kompyuta na ujuzi wa uongozi.

Ngurinuje Tjivikua, mwanafunzi katika shule ya Rocky Crest mwenye umri wa miaka 20 aliyejiunga katika masomo ya juu ya sekondari mwaka jana, anakumbuka uzoefu ambao umeweza kubadili maisha akisema,“pale ilikuwa ni michezo ya kompyuta, yaani vitu vinavyojongea, lakini kilichotufurahisha ilikuwa ni wakati tulipojifunza jinsi ya kuliuza wazo lako. Mimi ni muongeaji sana lakini nilikuwa siwezi kusimama mbele ya watu na kusema mawazo yangu. Baada ya kujifunza hivyo nikaelewa kuwa ninataka kufanya zaidi, ninataka kuongea zaidi kuhusu yale ninayoyafahamu na kwa kuwa tunatumia lugha tofauti na kulikuwa na watu wa tofautitofauti ambao tulikuwa tunawaeleza mawazo yetu nikagundua ninaweza kuongoza, ninataka kuongoza na ninataka kufahamu zaidi.”  

Aidha Ngurimuje Tjivikua ametoa ushauri kwa wasichana wenzake akisema,“badala ya kuwa na wasichana wadogo wanazunguka tu mtaani wanatakiwa kujifunza kuhusu programu za kompyuta kwasababu asilimia 90 ya kazi zote za siku za usoni zitahitaji ujuzi wa teknolojia ya mawasiliano na Habari na ni asilimia 28.4 tu ya watu wote wanaojiuhusha na sayansi, teknolojia,  uhandishi na hisabati (STEM) ni waanawake na ni asilimia 30 tu katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara huku ikiaminika kuwa Kwa hivyo ndiyo wasicaha zaidi wanatakiwa kujifunza kuhusu programu hizi.”

Katika hafla fupi ya kukabidhiwa Kompyuta mpakato kwa kila msichana, Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Namibia kwa kushirikiana na Wizara ya elimu, Sanaa na utamaduni ya Namibia walifanikisha tukio hilo ili kuonesha uungaji wao mkono kwa wasichana hao wataalamu wa Kompyuta.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Namibia, Bi Rachel Odede amewapongeza wasichana hao  kwa kukamilisha programu hiyo na kuiwakilisha Namibia. Kupitia hotuba yake, amesema, “ikiwa wasichana wadogo na wanawake hawana mafunzo na nafasi ya kuifikia teknolojia ya mawasiliano, wataachwa nyuma. Kuwafundisha wasichana utaalamu wa teknolojia ya kopyuta, kunahitajika ili kuondoa pengo katika dunia ya teknolojia na mgawanyiko wa kijinsia katika dijitali.”

Aidha Bi Odede akiwahamasisha wasichana kuendelea kuziamini ndoto zao, amenukuu alichosema muigizaji Lupita Nyongo mwaka 2014 akipokea Tuzo ya Oscar aliposema, “bila kujali unakotokea, ndoto zako ni halali.”

Naye Edda Bohn, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sanaa na Utamaduni amewasihi wasichana kuifikia jamii hususani vijana waliko nje ya shule ili waweze kuuutumia ujuzi wao mpya na kuurejesha katika ujifunzaji. Amesisitiza ushirikiano mzuri kati ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Namibia katika kuwezesha fursa muhimu Zaidi ya vitabu kwa wasichana wa Namibia.

Duniani ni asilimia 28.4 tu ya watu wote wanaojiuhusha na sayansi, teknolojia,  uhandishi na hisabati (STEM) ni waanawake na ni asilimia 30 tu katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara huku ikiaminika kuwa asilimia 90 ya kazi zote za siku za usoni zitahitaji ujuzi wa teknolojia ya mawasiliano na Habari.