Vikwazo vya ununuzi wa silaha vinaendelea CAR-Baraza la usalama

31 Januari 2020

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo tarehe 31 limepitisha azimio lilowasilishwa na Ufaransa kuendelea kuiweka vikwazo vya ununuzi ya silaha Jamhuri ya Afrika ya kati.

Akizungumza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, Balozi wa Ufaransa Anne Gueguen amesema, “ pamoja na hali ya kuendelea kutetereka kwa usalama, tunadhani ni muhimu kudumisha mfumo wenye uwajibikaji na kuhakikisha kwamba tunawasisitiza viongozi wakuu wa Afrika ya Kati katika maendeleo yao kuelekea kuleta mageuzi katika sekta ya usalama, na kuelekea kunyang’anya silaha na kujumuishwa kwa wanachama wa zamani wa makundi ya kujihami kwa silaha na pia usimamizi bora wa silaha.”

Amerejelea kwa kusema azimio ni “jambo muhimu kwa kurejesha amani na usalama katika Jamhuri ya Afrika ya Kati," na kwamba nchi yake "itaendelea kutoa msaada wowote kwa mamlaka kuu za CAR ili kufanikisha hilo."

Balozi wa Urusi Dmitry Polyanskiy, ambaye katika upigaji kura hakushiriki kuonesha msimamo wowote ameliambia Baraza, “tulitete ulengezwaji wa vikwazo. Bahati mbaya si viongozi wa Bangui au msimamo wetu ambao ulitiliwa maanani.”

Ameendelea kueleza kuwa, “vikwazo vya ununuzi wa silaha dhidi ya CAR vingweza kuwa na faida katika hatua za mwanzo, hata hivyo, kwa sasa uamuzi huu ni kikwazo kuweza kulipatia silaha jeshi la taifa na vikosi vya usalama, ambazo ni taasisi muhimu zenye jukumu muhimu la kuhakikisha usalama na amani ya raia wao. Kwa sasa, makundi yenye kujihami, na wavurugaji wa mchakato wa amani hawana vikwazo linapokuja suala la kupata silaha kupitia njia za magendo.”

Balozi wa CAR katika Umoja wa Mataifa Ambroisine Kpongo, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, “shughuli zinazofanywa na makundi yenye silaha kaskazini mwa nchi, hasa katika Mkoa wa Vakaga bado ni chanzo cha wasiwasi mkubwa watu.”

Amesema, “kuwapatia vikosi vya ulinzi na usalama magari kutawasaidia kuweza kusafiriki kutoka eneo moja hadi jingine ambako kumeathirika  na ukosefu wa usalama na kuruhusu kuingilia kati kuwalinda watu. Ni kwa sababu ya shughuli za hao wahalifu zinaweza kuonekana katika kwa kiasi tofauti katika nchi, serikali inasihi kuondolewa kabisa kwa vikwazo vya ununuzi wa silaha.”

Kura zilizopigwa, 13 zimeliunga mkono azimio la kuendelea kwa vikwazo, na mbili kati ya hizo hazikuonesha msimamo.

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter