Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jaribio la elimu bora ulimwenguni, linakabiliwa na changamoto kubwa

Wasicana wadogo wakirejea nyumbani baada ya masomo katika mji wa Bol nchini Chad
UN Photo/Eskinder Debebe)
Wasicana wadogo wakirejea nyumbani baada ya masomo katika mji wa Bol nchini Chad

Jaribio la elimu bora ulimwenguni, linakabiliwa na changamoto kubwa

Utamaduni na Elimu

Kuunganisha ushirikishaji, elimu bora na malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, vilikuwa sehemu kubwa ya mjadala wa leo wakati Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Tijjani Muhammad Bande alipoendesha mkutano kuhusu siku ya kimataifa ya elimu.

“Sekta ya elimu inapambana na changamoto nyingi sana duniani kote,” amesema Balozi Muhammad Bande.

Akizitaja changamoto hizo, Balozi Bande amesema kuna anguko katika ubora na viwaango vya elimu, kuongezeka kwa pengo kaati ya wanafunzi katika nchi ambazo zimeendelea na zile ambazo zinaendelea; janga la kujifunza kaatika maeneo ya migogoro; kuongezeka kwa uonevu wa shuleni, na kushuka kwa ari ya taaaluma ya ufundishaji kiujumla.

Grace Kaneiya
Bila elimu ni vigumu kufikia malengo hayo mengine-Muhammad-Bande

 

Bwana Muhammad-Bande ameendelea kueleza kuwa elimu ya sasa inapaswa, “kuziba pengo lililoibuka kati ya maahitaji ya sasa ya ajilaa zaa kisasa kwa ajili ya ujuzi maalumu, na fursa halisi za kujifunza. Mitaala bado  kutarajia na kujibu mahitaaji mahali pa kazi, ufundi, matumizi ya teknolojia wakati bado inaendeleza harakati za masomo yaa jadi.” Balozi Bande amesisitiza.

Elimu katika migogoro

Hatima ya watoto waliokwama katika maeneo ya migogoro inastahili kuangaliwa zaidi

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, katika mwaka 2017, mashambulizi 500 yalifanyika katika shule katika nchi 20 duniaani kote. Katika nchi 15 kati ya hizo 20, vikosi vya kijeshi na vikosi vya waasi waliyageuza madarasa kuwa vituo vya kijeshi.

Maelfu ya watoto walichukuliwa kuwaa wapiganaji, na wakati mwingine walifanywa kwenda kujitolea kufa kwa kujilipua na mabomu aau hata kulazimishwa kutekeleza mashambulizi ya moja kwa moja.

Wakati huo huo majanga ya asili nayo yanaongeza vitisho kwa mazingira ya kujifunzia. Vimbunga na dhoruba ni miongoni mwa hali ya hewa ambayo mara kwa mara vimesababisha mataatizo katika majengo ya shule na hivyo kufanya ujifunzaji kuwa mgumu kama siyo kutowezekana kaabisa.

Nguvu ya elimu

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed akihutubia mkutano huo amesema “Elimu ina nguvu ya kuiweka vizuri dunia,”

“Elimu inawalinda wanaume na wanawake dhidi ya unyonyaji katika soko la ajira na inawapa nguvu wanawake na kuwapatia fursa za kuchagua.” Amesisisita Bi Mohammed.

Wekeza katika elimu

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa upande wake limesema linasherehekea ushawishi mkubwa wa elimu katika kuunga mkono watu, ustawi, duniani na amani ingawa bado ni rasilimali ambayo ni haba kwa mamilioni ya watu ulimwenguni kote.