Bila elimu ni vigumu kufikia malengo hayo mengine-Muhammad-Bande 

24 Januari 2020

Leo Januari 24 ni siku ya elimu duniani ambapo Umoja wa Mataifa umeungana na dunia kuadhimisha siku hii muhimu.

Katika ujumbe wake kwa siku hii rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Tijjani Muhammad-Bande amesema, ‘Katika siku hii ya kimataifa ya elimu, ningependa kuhimiza sisi sote kufanya kila tuwezalo kwa ajili ya kuhakikisha elimu bora kwa wote."

Bwana Muhammad-Bande amesema elimu ni kipaumbele kwa dunia na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 limeweka lengo hilo kama lengo la nne.

Rais huyo wa Baraza Kuu amesema, “bila elimu ni vigumu kufikia malengo hayo mengine. Elimu inarahisisha uwezekano wa kuvumilia wengine, kuelewa tamaduni zingine. Inarahisisha uwezekano wa kupata ajira na kusalia na ajira hiyo, inarahisisha ubunifu wa mtu na inawezesha mtu kuishi na watu wengine katika njia sahihi. Elimu ni kila kitu."

Bwana Muhammad-Bande amehitimisha ujumbe wake kwa kusema, “katika elimu kadri tunavyoshirikiana, ndivyo tunakuwa bora hususan kwa sababu elimu sio tu kwa kiwango cha taifa, Elimu kwa sababu inauhusiano na maarifa haina mwisho. Kila mtu anaweza kujifunza mengi kila siku."

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter