Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali bado ni ya wasiwasi japokuwa mauaji dhidi ya waandishi wa habari yamepungua

Wanahabari wakifuatilia kuwasili kwa viongozi kwenye mlo wa faragha wa kila mwaka unaoandaliwa na Katibu Mkuu wa UN
UN /Rick Bajornas
Wanahabari wakifuatilia kuwasili kwa viongozi kwenye mlo wa faragha wa kila mwaka unaoandaliwa na Katibu Mkuu wa UN

Hali bado ni ya wasiwasi japokuwa mauaji dhidi ya waandishi wa habari yamepungua

Haki za binadamu

Ripoti ya UNESCO iliyotolewa hii leo mjini Paris Ufarasansa inasema ingawa idadi ya waandishi wa habari waliouawa duniani kote imepungua kwa takribani nusu katika mwaka 2019, wanahabari wanakabiliana na hatari zinazoendelea na watekelezaji wa matukio hayo wanaonekana kutowajibishwa kutokana na matendo yao.

Uchunguzi wa UNESCO wa wanahabari waliouawa, ilirekodi vifo 56 vya wanahabari mnamo mwaka 2019 ikilinganishwa na vifo 99 katika mwaka 2019, ikiwa ni kiwango cha chini kuwaahi kutokea karibia katika muongo mzima.

Kwa ujumla, UNESCO umerekodi mauaji ya waandishi wa habari 894 katika muongo mmoja wa mwaka 2010 hadi 2019, ambao ni wastani wa asilimia 90 kwa mwaka.

Waandishi wa habari waliuawa katika maeneo yote duniani, Amerika ya kusini na Karibea ikirekodi mauaji 22, idadi hiyo ikiwa ni kubwa ikifuatiwa na vifo 15 vya Asia-Pasifiki na vifo 10 katika mataifa ya kiarabu.

Waandishi wengi wa habari waliuawa nje ya maeneo ya mizozo

Takwimu zinaonesha kuwa waandishi wa habari siyo tu wanakuwa katika hatari kubwa wakati wanapofuatilia na kuripoti matukio ya vurugu, lakini pia wanalengwa wanaporipoti siasa za nchi zao, rushwa na uhalifu, mara nyingi katika miji yao.

Karibia theluthi mbili yaani asilimia 61 ya visa katika mwaka 2019 vilitokea katika nchi ambazo hazina migogoro, kikiwa ni kiwango cha juu katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni kurejea nyuma ikilinganishwa na mwaka 2014 wakati ambapo visa vilikuwa theluthi moja.

UNESCO inajitolea kwa ajili ya usalama wa waaandishi wa Habari

Akizungumzia takwimu hizi, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay amesema, "UNESCO bado inasikitishwa sana na uhasama na vurugu zinazoelekezwa kwa waandishi wa habari wengi ulimwenguni. Kadiri hali hii inavyodumu, itapunguza mjadala wa demokrasia."

UNESCO inafanya kazi kuboresha usalama wa waandishi wa habari na kupambana na ulinzi kwa uhalifu dhidi ya wanahabari ikiwemo kwa kuongoza utekelezaji wa Mpango wa Utendaji wa UN kuhusu usalama wa waandishi wa habari na suala la kulindwa kwa wahalifu.