Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waathirikwa wa tetemeko la miaka 10 iliyopita Haiti waenziwa na UN

Katibu Mkuu wa UN António Guterres ahudhuria Maadhimisho ya Makumbusho ya Kumi ya mtetemeko ya ardhi ya Haiti ya tarehe 12 Januari 2010
UN Photo/Evan Schneider
Katibu Mkuu wa UN António Guterres ahudhuria Maadhimisho ya Makumbusho ya Kumi ya mtetemeko ya ardhi ya Haiti ya tarehe 12 Januari 2010

Waathirikwa wa tetemeko la miaka 10 iliyopita Haiti waenziwa na UN

Tabianchi na mazingira

Zaidi ya watu 200,000 waliopoteza maisha wakati tetemeko kubwa lilipokikumba kisiwa cha Haiti miaka 10 iliyopita leo wameenziwa katika sherehe maalum ya kumbukumbu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New york ikijumuisha pia wafanyakazi 102 wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha pia ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya wafanyakazi kufa katika tukio moja kwenye historia ya Umoja wa Mataifa.

Katika hafla hiyo akiweka shada la maua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekumbusha kwamba “Wahaiti walianza mwaka mpya na matumaini mapya lakini katika dakika chache matumaini yao yaligeuzwa vumbi. Sitasahau mshituko nilioupata na huzuni iliyotanda kote duniani na kwenye Umoja wa Mataifa wakati ukubwa wa janga hilo ulipokuwa ukitambulika.”

Ameongeaza kuwa ingawa 12 Januari 2010 ilikuwa moja ya siku zenye kiza totoro katika historia “Haiti ilitegenea ujasiri na  dhamira ya watu wake na msaada kutoka kwa marafiki zake. Barabara zilikarabatiwa, nyumba zikajengwa, shule zikafunguliwa , na biashara zikaanza tena.”

Mji mkuu wa Haiti , Port-au-Prince uliharibiwa sana na tetemeko la ardhi la Januari 2010.
UN Photo/Marco Dormino
Mji mkuu wa Haiti , Port-au-Prince uliharibiwa sana na tetemeko la ardhi la Januari 2010.

 

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alichukua muda wa hotuba yake kukumbuka nyanja mbalimbali za juhudi za Umoja wa Mataifa Haiti ambazo zimesababisha machungu zaidi badala ya faraja, akikumbuka mlipuko wa kipindupindu ambao alianza mwaka 2010, ukiaminika kwa kiasi kikubwa kwamba uliingizwa nchini humo na walinda amani.

Katibu Mkuu amesema “Miongoni mwa changamoto ambazo Umoja wa Mataifa unazijutia ni kupotea kwa maisha ya watu na madhila yaliyochangiwa na mlipuko wa kipindupindu. Nakaribisha hatua zilizopigwa ambazo zimesaidia kutokomeza ugonjwa huo.Pia tumejizatiti kutatua changamoto ambazo hazijshughulikiwa za ukatili na unyanyasaji wa kingono.”

Katibu Mkuu ametoa wito kwa watu wa Haiti kutatua tofauti zao kupitia majadiliano na kujizuia na mivutano zaidi ambayo inaweza kubadili hatua nyanya zilizopigwa katika muongo uliopita.

Amesema ofisi mpya ya Umoja wa Mataifa Haiti (BINUH) umechukua nafasi ya mpango wa operesheni za ulinzi wa amani uliodumu kwa miaka 15 na mashirika 19 na mipango , mifuko na programu zilizopo nchini humo “zitaendelea kufanyakazi kwa ushirikiano na watu wa Haiti katika mchakato wa ujenzi mpya na mafanikio.”

Ukumbusho wa Tetemeko la ardhi la Haiti 2010 unajengwa katika Makao makuu ya UN na vipande vya taka kutoka Hoteli ya Christopher Port-au-Prince kuzikwa katika msingi wa eneo la kumbukumbu.
UN Photo/Mark Garten)
Ukumbusho wa Tetemeko la ardhi la Haiti 2010 unajengwa katika Makao makuu ya UN na vipande vya taka kutoka Hoteli ya Christopher Port-au-Prince kuzikwa katika msingi wa eneo la kumbukumbu.

 

UN ilipoteza watu toka nchi 30

Kabla ya sherehe hiyo ya kumbukumbu Katibu Mkuu alizuru kile kilichoelezewa kuwa ni ‘’makumbusho mapya yaliyohamishwa yaitwayo A Breath , ambayo sasa yamewekwa kwenye makao makuu mjini Manhattan yakiwa yamewasili kutoka mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince. ‘’Namshukuru mchongaji Davide Dormino na kila mtu aliyesaidia kuyasafirisha hadi hapanimevutiwa sana na kujumuisha kifusi kutoka kwenye hotel ya Christopher ambako wafanyakazi wenzetu wengi walipoteza maisha ‘’.

Guterres amesema wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliokufa walikuwa nchini Haiti ‘’kusaidia kurejesha utulivu na kuleta mafanikio, na pia kudumisha amani na usalama na washirika wa kimataifa, kitaifa na wenyeji. Miongoni mwao walikuwepo washauri wa sera, maafisa wa kisiasa, wahudumu wa kibinadamu, wataalam wa maendeleo, maafisa usalama, wanajeshi, wanasheria, madereva na madaktari. ‘’

Wakati tetemeko lililipotokea wafanyakazi wengi wa Umoja wa Mataifa walishiriki katika uokozi na kubeba majeruhi hadi kwenye makazi ya Umoja wa Mataifa . Na wengine walikabiliwa na kibarua kigumu cha kusafirisha maiti  za wafanyakazi wenzao hadi nyumbani kwa wapendwa wao kwa ajili ya mazishi na wengine kuchomwa . Janga hilo liliwaleta karibu watu wa Haiti na Umoja wa Mataifa amesema Katibu Mkuu na halisani hatosahau. Akaongeza kuwa “Njia bora ya kuwaenzi waliopoteza Maisha ni kufanya kazi kwa pamoja na wat una serikali ya Haiti, marafiki wa Haiti na waungaji mkono wao katika jumuiya ya kimataifa. Kwa pamoja tutalinda na kuhakikisha mustakabali bora wa Haiti na ujenzi wa amani, mafanikio na utu kwa Wahaiti wote.”

Lazima kuendeleza mshikamano

Akizungumza kwa niaba ya serikali ya Haiti katika kumbukumbu hiyo kutoka kwenye mpango wa Haiti kwenye Umoja wa Mataifa Patrick Saint-Hilarie amesema “Miaka 10 baadaye dalili za tetemeko hilo bado ni Dhahiri kila kona ya Haiti.Watu jasiri wa Haiti bado wanalipa athari ambazo zimeighubika Haiti tangu wakati huo”

Akiushukuru Umoja wa Mataifa na wote walioshikamana na Haiti wakati wa zahma hiyo amesema “Hivi sasa ni juu ya watu wa Haiti kwanza kabisa kuchukua jukumu la changamoto zinazotukabili hibi sasa na kisha kuchukua hatua Madhubuti na za lazima kuboresha hali ya taigfa letu. Leo hii kuliko wakati mwingine wowote nchi yetu inahitaji kuendelea na mshikamano wa kitaifa, kimataifa na kutimiza kwa nguvu zote matakwa ya watu wa Haiti.”

Amesema bado kuna kibarua kikubwa cha kufanyana kwamba “tukiadhimisha kumbukumbu ya miaka 10bado hatujachelewa kuibeba changamoto ya kukamilisha ujenzi mpya wa Haiti.”