Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kimbunga Idai kilitoa picha halisi ya hali ya watu wanoishi na ulemavu Zimbabwe:UNESCO

Waathirika wa kimbunga Idai na Kenneth nchini Msumbiji, Hap ni Beira mvulana akitizama kupitia dirisha ya darasa lake.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Waathirika wa kimbunga Idai na Kenneth nchini Msumbiji, Hap ni Beira mvulana akitizama kupitia dirisha ya darasa lake.

Kimbunga Idai kilitoa picha halisi ya hali ya watu wanoishi na ulemavu Zimbabwe:UNESCO

Tabianchi na mazingira

Wakati kimbunga Idai kilipiga nchi mbali mbali ikiwemo Zimbabwe kuna baadhi ya watu katika jamii hususan wanaoishi na ulemavu walikuwa hatarini na ilikuwa ni vigumu kwao kufikiwa na msaada, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO lililoandaa video mahsusi kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu suala hilo.

Hii ni sauti ya Tapiwa Sigauke ambaye ni mwenyekiti wa watu wenye ulemavu wa wadi ya Chimanimani, Zimbabwe anasema, wakati wa kimbunga baadhi ya watu walitupuuza, walituambia hawakuweza kutusaidia.

Kauli hiyo inaungwa mkono na watu wengi wanoishi na ulemavu walioko kijiji cha Chimanimani wakisema kwamba walihisi wametengwa wakati zahma hiyo ilipoghubika nchi yao.

Ili kubadili taswira na kujumuisha kila mtu katika kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma UNESCO inasema kunahitajika mkakati jumuishi. Mfano kunahitajika kuwepo sauti inayowakilisha mahitaji ya watu wanaoishi na ulemavu kama anavyosema Chamunowi Ringisayi, katibu wa chama cha watu waliopooza viungo Zimbabwe, Mutare

(Sauti ya Chamunowi)

« Sababu ambayo ilifanya Chimanimani ikajenga mijengo hiyo ambayo haifikiki ni kwa kuwa hakukuwa na mtu yeyote anayeishi na ulemavu ambaye angewapa ushauri kujenga majengo ambayo yanazingatia mahitaji ya watu wanoishi na ulemavu, kwa mfano sasa tumeshiriki katika mchakato wa ujenzi wa choo cha Ngangu, tulifanya kazi na wizara ya ujenzi wa umma na wamejenga choo kizuri. »

Lakini sio tu kwamba kunahitajika miundo msingi inayojali watu wanaoishi na ulemavu lakini pia vifaa stahiki kwa ajili ya usafiri wao, Bevy Munyare ni mwanakijiji Bikita.

(Sauti ya Bevy)

« Ninaishi na ulemavu, niaumuwa mara kwa mara, siwezi kutembea, hali imekuwa hivi maisha yangu yote, siwezi kutembea, ninahitaji kiti mwendo, ni kitu pekee ninachohitaji, kitarahisisha maisha yangu. »

Uwepo wa kimbunga Idai pia ulionesha hali halisi ya mfumo wa elimu ambayo sio jumuishi kwani kuna watoto ambao wanashindwa kuhudhuria shule kutokana na ukosefu wa miundo msingi kwa mfano kijana  Leslie Munaiwa junior ambaye hakuweza kuendelea na masomo yake ya sekondari.

Ansema, somo nililolipenda sana na lile la jumla, niliwaza kuendeleza masomo yangu lakini hilo halingewezekana, halingewezekana kwa ajili ya changamoto kadhaa.

Lakini ni nini suluhu kwa sasa? John Misi ni msimamizi wadi ya Chimanimani- 

(Sauti ya Misi) 

“Tunahitaji msaada, tunahitaji ushirikiano ambapo tutafanya uchunguzi kwa pamoja kutoka vijijini mpaka wilayani na tunahitaji programu ya elimu wilayani ili watu wanapoenda kuzungumza na watu wanoishi na ulemavu, tuhakikisha hatuingilii haki zao za msingi. Kwa hivyo tunahitaji mafunzo, tunahitaji raslimali na tunahitaji ushirikiano.”