Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali nchini Mali na ukanda wa Sahel, inazorota kwa kasi:UN

Walinda amani wa UN warejea kwenye helikopta yao kufuatia utume kwa kijiji cha Sobane Da katika eneo la Mopti wa Mali.
MINUSMA/Harandane Dicko
Walinda amani wa UN warejea kwenye helikopta yao kufuatia utume kwa kijiji cha Sobane Da katika eneo la Mopti wa Mali.

Hali nchini Mali na ukanda wa Sahel, inazorota kwa kasi:UN

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa leo umerejea ahadi yake mbele ya Baraza la Usalama ya kushirikiana n apande zote ili kushughulikia mizizi ya ugaidi, kutokuwepo na utulivu na machafuko nchini Mali na ukanda mzima wa Saheli.

Akikumbusha ahadi hiyo mbele ya kikao cha Baraza la Usalama kilichokuwa kikijadili hali ya Mali, mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amesema “Hali nchini Mali na ukanda mzima wa Saheli inazoroka kwa kasi ya kutia hofu”

Lacrois ameongeza kuwa wiki iliyopita walinda amani 18 wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali MINUSMA walijeruhiwa katika shambulio kwenye kambi ya Tissalit Kaskazini mwa nchi hiyo. Mbali ya tukio hilo amesema Alhamisi iliyopita  wanajeshi wengine 89 wa Nigeria waliuawa katika eneo la Chinagoder karibu na mpaka wa Mali katika shambulio ambalo Jumanne wiki hii kundi la kigaidi la ISS kwenye eneo la Grand Sahara lilidai kulitekeleza.

Na kama hiyo haitoshi amesema mnamo Januari 4 mwaka huu watoto 14 waliuawa katika shambulio kwenye basi karibu na mpaka baina ya Mali na Burkina Fasso eneo la Kaskazini.

Bwana Lacroix amewaambia wajumbe wa Baraza la Usalama kwamba makundi ya kigaidi yanaongezeka kushika kasi kwenye ukanda huo hasa katika majimbo ya Menaka na Gao nchini Mali. “Tumeshuhudia ongezeko la mashambulizi ya kigaidi kwa kutumia vifaa vya milipuko dhidi ya misafara yet una kusababisha vifo na majeruhi wengi miongoni mwa walinda amani na matukio haya yanatokea karibu kila siku. Magaidi wanaendelea kuchochea machafuko baina ya jamii Katikati mwa Mali” ameonya mkuu huyo na kuongeza kwamba hivi sasa kuna wakimbizi wa ndani wanaokabiliwa na njaa kubwa katika jimbo la Mpoti kuliko siku za nyuma.

Baraza la usalama likikutana na shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa
UN Photo/Loey Felipe
Baraza la usalama likikutana na shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa

 

Kwa Bwana Lacroix ameweka bayana kwamba kup[eleka vikosi vya mchanganyiko wa wanajeshi wa ulinzi wa Mali na vikosi vya usalama Kaskazini mwa Mali ni kipaumbele cha haraka na cha hali ya juu.

Mnamo tarehe 6 Januari mamlaka nchini Mali ilianza kupeleka kikosi cha kwanza mchanganyiko kutoka Bamako hadi Kidali kupitia Gao. Kikosi hicho kinatarajiwa kuwasili Kidali mwishoni mwa mwezi huu wa Januari. “Hii ni hatua muhimu sana katika kuelekea kurejesha udhibiti wa serikali nchini nzima” amesisitiza bwana Lacroix.

Rasilimali zaidi zinahitajika

Bwana. Lacroix amesema katika miezi ya hivi karibuni MINUSMA imefanya kila juhudi ili kutekeleza mkakati wake wa pili wa kipaumbele Katikati mwa Mali huku ikiendelea kuendesha shughuli zake zingine za kusaidia mkakati mkubwa kwa vipoaumble vilivyoweka kwa ajili ya eneo hilo la Kaskazini mwa nchi.

“Kuongezeka kwa shughuli na uwepo wa MINUSMA katika jimbo la Mopti kumesaidia kuzuia machafuko zaidi ya kijamii na kwa kiasi kikubwa mauaji.”

MINUSMA iliongeza kasi ya kujikita na Katikati mwa Mali , lakini ililazimisha mpango huo wa Umoja wa Mataifa kupeleka rasilimali kama za masuala ya anga, jeshi la kuchukua hatua haraka, masuala ya ujasusi, ufuatiliaji na udhibiti kutoka Gao Mopti.” Haiwezekani kwa MINUSMA kutekeleza vipaumbele vya ziada bila kuwa na rasilimali za kutosha “ ameonya bwana Lacroix

Mkuu wa Operesheni za Amani ya UN, Jean-Pierre Lacroix na Pedro Serrano, Naibu Katibu Mkuu wa Huduma ya Ulaya kwa Hatua za nje, watembelea mradi wa usalama wa uwanja wa ndege wa Mopti nchini Mali. Mradi huo unafadhiliwa na EU kwa msaada wa MINUSMA.
MINUSMA/Harandane Dicko
Mkuu wa Operesheni za Amani ya UN, Jean-Pierre Lacroix na Pedro Serrano, Naibu Katibu Mkuu wa Huduma ya Ulaya kwa Hatua za nje, watembelea mradi wa usalama wa uwanja wa ndege wa Mopti nchini Mali. Mradi huo unafadhiliwa na EU kwa msaada wa MINUSMA.

 

MINUSMA ni sehemu tu ya hatua za pamoja

Naye naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama amekumbusha kwamba “MINUSMA ni sehemu ndogo tu ya hatua kubwa za pamoja kukabiliana na ha tatizo la usalama, machafuko na mizizi yake nchini Mali na kwenye ukanda wa sahel  na kuwalinda raia.”

Ameongeza kuwa “Tunatiwa moyo na ahadi zilizodhihirishwa na wakuu wa nchi tano za Sahel (G-5) ambazo ni Burkina Fasso, Mali, Mautritania, Niger na Chad katika kupambana na ugaidi nchini Mali na katika ukanda mzima wa sahel kwa kushirikiana na wadau wengine wa kimataifa.