MONUSCO yasaidia kuzima moto mkubwa Butembo DRC na kuokoa maisha na mali

14 Januari 2020

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO Jumatatu Januari 13 ulisaidia kuzima moto mkubwa uliozuka katika kituo cha mafuta kisicho rasmi cha Clandestin kwenye mji wa Butembo Kivu ya Kaskazini.

Kwa mujibu wa posili wa MONUSCO kituo hicho cha matuta ni haramu na kipo kilikuwa katika nyumba moja kwenye wilaya ya Bwinyole manispaa ya Kimemi na kwa msaada wa MONUSCO hakuna mtu yeyote aliyepoteza Maisha au kujeruhiwa katika ajali hiyo ya moto.

Polisi wa MONUSCO walip[igiwa sim una kamanda wa jeshi la Congo mjini Butembo kuomba msaada na mara moja mkuu wa polisi wa MONUSCO Butembo aliwaarifu askari wa zimamoto wa MONUSCO ambao waliambatana na kikosi cha polisi walinda amani kutoka Misri hadi kwenye tukio ambako wakazi walikuwa wakijaribu kuzima moto huo bila mafanikio.

Polisi wa Congo (PNC) na polsi wa MONUSCo kwa kushirikiana na wakazi wa eneo hilo walishirikiana vyema na hatimaye kufanikiwa kuuzima moto huo baada ya saa takriban 6.

Moto huo licha ya kwamba haukukatili maisha ya mtu wala kujeruhi lakini umesabbaisha uharibifu mkubwa na uchunguzi unaendelea kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la polisi la congo , PNC.

Raia wa Butembo wamekaribisha mchango wa MONUSCO ambao ulisaidia kuzuia kusambaa kwa moto huo ambao umezusha maswali mengi kuhusu kujirudia kwa vitemndo vya kutotimiza masharti ya viwango vya usalama dhidi ya uuzajoi haramu wa mafuta na moto mjini Butembo.

Biashara hiyo haramu ya mafuta mara nyingi hufanyika popote ikiwemo majumbani ikikiuka kanuni za usalama, na kuhatarisha Maisha ya wat una mali zao.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter