Mabadiliko ya tabianchi yanaleta changamoto kubwa kwa wanawake wavuvi Ecuador:WFP

14 Januari 2020

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa nchini Ecuador hasa kwa wanawake wanaotegemea na kufanya kazi ya uvuvi. 

Huyo ni mmoja wa mamia ya wanawake wavuvi wanaopitia changamoto kubwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi nchini Ecuado. Elivia Valencia mwenye umri wa miaka 24 anaishi kwenye kisiwa cha Palma Real kwenye mpaka baina ya Ecuador na Colombia , ni kisiwa kidogo ambacho wanawake wengi wanaishi kwa kazi ya uvuvi wa samaki na kuuza makombe.

Kazi yao kwa mujibu wa Elvia inategemea sana hali ya hewa, “mabadiliko ya tabianchi yametuletea changamoto kubwa tusiyoikaribisha, wakati wa msimu wa ukame makombe yanaanza kufa kwa sababu ya kukosa mvua  na hiyo inatuathiri sana sisi , kwa nini? Kwa sababu labda tuseme kati ya dola 8 unazopata kwa siku ni kwa ajili ya kutulisha, karo ya shule, nguo na sisi kuweza kuishi. Tatizo ni kutopata fedha za kutosha kuweza kununua chakula.”

Elivia anaongeza kuwa wakati mwingine wanakosa hata hela ya kununua chakula kwa sababu hakuna makombe ya kutosha .

Na Ecuador wanawake ndio waathirika zaidi wa mabadiliko haya ya tabianchi kuliko wanaume kwa sababu,“Sisi ndio wawajibikaji wakati mwingine wanaume wanaondoka na sisi ndio tunaobeba jukumu la watoto wetu na kuangalia nyumba zetu, ndio tunaoathirika zaidi na kinachotokea.”

Hivi sasa WFP imeanzisha juhudi za kuwasaidia wanawake hawa hasa kwa mgao wa chakula inapobidi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud