Kumepigwa hatua muhimu kuelekea amani Colombia- Massieu

13 Januari 2020

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Colombia Carlos Ruiz Massieu amesema katika kipindi cha mwaka uliopita, Colombia imeendelea kupiga hatua muhimu katika mchakato wa amani wakati ikikabiliwa na changamoto nyingi hususan katika maeneo ambako jamii imeathiriwa na vita, usalama wa viongozi wa jamii na waasi wa zamani.

Akihutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu kuhusu maendeleo nchini Colombia bwana Massieu ameonya kuhusu hatari kwa amani akisema, “ukatili uliotapakaa katika maeneo yaliyoathirika na mzozo inaendelea kutishia amani kama inavyoashiriwa na matukio ya kusikitisha ya hivi majuzi.”

Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu amesema, “tangazo la jana na mamlaka kwamba wamezuia shambulio la kumuua rais wa kundi la waasi la FARC Rodrigo Londoño, almaarufu kama 'Timochenko' inaashiria hatari ya waliokuwa wanachama wa FARC na mchakato wa amani na umuhimu wa kuhakikisha usalama wake.

Ameongeza kwamba visababishi vya ukatili vimeangaziwa katika sehemu mbali mbali za makubaliano ya amani na hiyo ni moja ya sababu kubwa ya kuhakikisha utekelezaji wake.

Watu muhimu katika kufanikisha amani

Kuhusu hatua zilizopigwa katika kusongesha mbele amani, bwana Massieu ametoa shukran kufuatia ushiriki wa serikali ya Colombia, FARC, ushirikiano kutoka kwa jamii ya kimataifa na watu wa Colombia ambao kila siku hufanya bidi katika kuimarisha amani katika jamii zao.

Carlos Ruiz Massieu,mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu na mkuu wa mpango wa uhakiki wa Umoja wa Mastaifa nchini Colombia (UNVMC)akitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
UN Photo/Eskinder Debebe)
Carlos Ruiz Massieu,mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu na mkuu wa mpango wa uhakiki wa Umoja wa Mastaifa nchini Colombia (UNVMC)akitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Akitolea mfano juhudi hizo amesema, “ongezeko la ushirika na kumarika kwa usalam katika chaguzi za kikanda ni ishara ya athari chanya za mchakaro wa amani katika demokrasia ya Colombia. Tume ya Ukweli, Haki, msamaha na kutorudia iliendelea na kazi yake muhimu, na ushirika wa waathirika. Maelfu ya waasi ambao walikuw ana silaha miaka michahce iliyopita wanaendelea kujena Maisha yao kupitia fursa zitokanazo na uwepo wa amni licha ya changamoto nyingi na hatari.”

Bwana Massieu amesisitiza kwamba ni lazima hatua zilizopigwa kulindawa, kuhifadhiwa na kutumika na njia nzuri ya kufikia hili ni kupitia utekelezaji jumuishi wa mkataba wa amani.

 Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaunga mkono safari ya amani

Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu amekubusha kwamba Desemba 27 barabara kuelekea ujumuihswaji ilipitishwa ambayo inatoa muongozo wa mchakto wa muda mrefu wa ujumuishwaji na kwamba Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unalenga kuunfa utekelezaji wake mkono.

Ameongeza kwamba waliokuwa waasi 2,500 wananufaika na miradi 12 ya pamoja lakini kando na ufadhili na uendeshaji wake, “ni muhimu kuhakikisha uwepo wake kwa muda mrefu na kuwa endelevu ikiwemo ufikiaji wa ardhi, msaada wa kiufundi na ufikiaji wa soko.”

Hatimaye ameelezea umuhimu wa kuzingatia waliokuwa waasi 9,000 ambao wanaishi maeneo ya nje kwa sababu wanakabiliwa na hatari kubwa na vikwazo zaidi katika kufikia huduma za msingi na fursa za elimu, ajira na uzalishaji na zaidi ya watoto 2000 ya waliokuwa waasi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter