Guterres aelezea wasiwasi wake kufuatia ongezeko la uhasama Sahara magharibi

Walinda amani wakikagua eneo baada ya amri ya kusitisha mapigano huko Smara Sahara Magharibi.
UN Photo/Martine Perret
Walinda amani wakikagua eneo baada ya amri ya kusitisha mapigano huko Smara Sahara Magharibi.

Guterres aelezea wasiwasi wake kufuatia ongezeko la uhasama Sahara magharibi

Amani na Usalama

Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea wasiwasi wake Jumamosi kufuatia ongezeko la uhasama Sahara magahribi wakati huu ambapo mashindano ya gari Afrika yanavuka kijiji cha Guerguerat.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa wadau kujizuia na kupunguza uhasama wowote.
Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, bwana Guterres amesema ni muhimu kuwacha raia na magari kupita bila kuzuiwa na i muhimu kujizuia na vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kubadili hali kama ilivyo kwenye maeneo yanayotunzwa kwa ajili ya kuhakikisha hali bora ya hewa, udongo na maji na kuzuia changamoto mbalimbali za kimazingira.

Taarifa ya Katibu Mkuu imemnukuu akirejelea dhamira ya Umoja wa Mataifa kuunga mkono pande husika katika kufikia suluhu ya kisiasa yenye haki, ya kudumu na inayokubalika na wote kwa ajili ya mzozo wa Sahara magharibi kwa mujibu wa maazimio ya Baraza la Usalama