Katibu Mkuu atuma rambirambi kwa familia na watu wa Oman kufuatia kifo cha Sultan Qaboos

11 Januari 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres  ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya kifalme, serikali na watu wa Oman kufuati kifo cha Sultan Qaboos Said ambaye alifariki usiku wa Ijumaa akiwa na umri wa miaka 79.

“Sultan Qaboos aliongoza Oman kwa kipindi cha miaka 50 na alikuwa mstari wa mbele katika kubadilisha Oman kuwa nchi iliyoendelea na yenye utulivu,” amesema Katibu Mkuu kupitia tarifa yake iliyotolewa na msemaji wake.

Bwnaa Guterres amesema Sultan alikuwa amedhamiria kueneza ujumbe wa amani, uelewano na kuishi pamoja katika ukanda huo na kimataifa, na kuheshimika na watu katika ukanda huo na kwingineko.

Taarifa ya Katibu Mkuu imemnukuu akitoa shukrani zake kwa Sultan kwa mchango wake katika nyanja ya diplomasia ukanda huo na kimataifa.

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud