Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katiba ya UN ikikaribia miaka 75, Baraza la Usalama laahidi kuidumisha

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wakiwa wameshikilia nakala za Katiba ya Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya UN New York
UN Photo/Amanda Voisard
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wakiwa wameshikilia nakala za Katiba ya Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya UN New York

Katiba ya UN ikikaribia miaka 75, Baraza la Usalama laahidi kuidumisha

Amani na Usalama

Katika kuelekea maiak 75 ya Umoja wa Mataifa itakayoadhimishwa baadaye mwaka huu , Baraza la Usalama la Umoja huo limeahidi dhamira yake ya kudumisha katiba ya Umoja wa Mataifa ambayo ndio nguzi ya kuanzishwa kwa Umoja huo na pia kwa utulivu wa kimataifa kwa msingi wa sheria za kimataifa.

Katika tarifa yao iliyotolewa na rais wa Baraza hilo leo Alhamisi, kwenye mjadala wa wazi kuhusu wajibu wa katiba hiyo katika kuhakikisha amani na usalama wa kimataifa, wajumbe 15 wa Baraza la Usalama wamesisitiza “Dhamira ya kuhakikisha ushirikiano wa kimataifa na kwa jukumu kuu la Umoja wa Mataifa”.

Umuhimu wa Katiba ya UN

Rais huyo wa Baraza amesema “Baraza la Usalama linatambua umuhimu mkubwa wa katika katika kudumisha amani na usalama wa kimataifa na maendeleo ya sheria za kimataifa, ikiwemo mingingi ambayo inaendesha ushirikiano baina ya mataifa kwa mtazamo wa kusaidia kuzuia kuzuka kwa vita.”

Ameongeza kwamba ni nyongeza ya azimio lililopitishwa mwanzo wa mjada kuhusu katiba.

Baraza la Usalama limekumbusha kwamba katina hiyo imelipa Baraza jukumu la msingi kwa ajili ya kuhakikisha amani na usalama wa kimataifa na kwa mantiki hiyo Baraza linasisitiza kwamba “Mataifa yote , na mashirika yote ya kimataifa na ya kikanda na mengine ni lazima yaheshimu hilo.”

Baraza limetoa witoo kwa nchi zote wanachama kuheshimu katiba hiyo na kuichagiza na kuitetea.

Mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu udumishaji amani na usalama wa kimataifa na kudumisha Katiba ya Umoja huo
UN Photo/Mark Garten)
Mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu udumishaji amani na usalama wa kimataifa na kudumisha Katiba ya Umoja huo

Ushirikiano wa kimataifa uko njia panda-Guterres

Wakati wa mjadala huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kwamba mwaka mpya umeanza kwa misukosuko hususan katika ukanda wa Ghuba na kwamba “Kuaminiana ndani na miongoni mwa mataifa kunatoweka huku kukiwa na ongezeko ya mivutano nje ya miapaka. Ushirikiano wa kimataifa nao uko njia panda , yote haya yanaendeleza mtohani mkubwa wa kupima ushirikiano wa kimataifa”.

Guterres ameongeza kuwa “Kipindi hiki ni cha migawanyiko na kutokuwa na utulivu kimataifa, na katiba inasalia kuwa ndio muongozo wa wa ushirikiano wa kimataifa na kwa maslahi yetu sote. Katika zama za kusambaa kwa chuki na ukwepaji sheria , katiba inatukumbusha sote jukumu la msingi la utawala wa sheria na utu wa binadamu”.

Na Guterres ameongeza kuwa “ Na katika zama hizo za mabadiliko ya haraka na mabadiliko ya teknolojia , tahami na malengo ya katiba yanaendelea kutatua kwa amani migogoro, kuhakikisha usawa baina ya wanawake na wanaume, kutoingilia uhuru, haki ya kujitawala na uhuru wa usawa miongoni mwa nchi wanachama na sheria zilizo bayana zinazotoa muongozo kuhusu matumizi ya nguvu.”

Kutekeleza matakwa ya katiba

Kwa mujibu wa mkuu wa Umoja wa Mataifa changamoto iliyopo ni “Kufanya juhudi zote kutekelezwa malengo ya katiba na kutimiza ahadi yake kwa ajili ya vizazi vijavyo”

Antonio Guterres amesema “endapo katiba ya Umoja wa Mataifa na malengo na misingi yake bado ni thabiti hii leo basi nyenzo zetu lazima ziende sanjari na hali halisi ya sasa, na tunapaswa kuzitumia kwa umakini zaidi na ubunifu.”

Katibu Mkuu anaamini kwamba moja ya nji bora ni kuwekeza katika kuzuia. “Tunatumia muda mwingi na rasilimali katika kudhibiti na kukabiliana na migogoro kuliko kuizuia. Mtazamo wetu unahitaji kupimwa tena”.

Kisha akatoa wito wa kutambua kwamba malengo ya maendeleo endelevu ni miongoni mwa nyenzo bora za kuzuia. “Natoa wito kwa nchi zote wanachama kuwekeza Zaidi katika ajenda ya maendeleo endeleyo ya 2030 hususani usawa wa kijinsia, ujumuishwaji, utangamano katika jamii, utawala bora na utawandawazi wenye usawa ambao utakhakikisha haki za kila mtu, talanta ya kila mt una kumshirikisha kila mtu katika jamii.”