Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa FAO wa kukabiliana na jangwa wazaa matunda Burkina Faso

Kufuatia ,mabadiliko ya tabianchi ukame wa mara kwa mara unatishia usalama wa chakula.
©FAO/Giulio Napolitano
Kufuatia ,mabadiliko ya tabianchi ukame wa mara kwa mara unatishia usalama wa chakula.

Mradi wa FAO wa kukabiliana na jangwa wazaa matunda Burkina Faso

Tabianchi na mazingira

Mradi wa kimataifa wa kukabiliana na jangwa ulioashindwa na shitrika la Umoja wa Mataifa la chakula la kilimo FAO umeanza kuleta nuru kwa wakulima nchini Burkina Faso

Tangu mwaka 2016 FAO na washirika wake wamechukua hatua kuzisaidia nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Burkina Fasso ambayo inakabiliwa na hali mbaya kutokana na ukame wa muda mrefu na mabadiliko ya tabianchi.

Hatua hizo ni kuendesha mradi wa hatua dhidi ya jangwa (AAD) mradi ambao unajumuisha bara la Afrika , nchi za Caribbea na Pasifiki  kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya.

Lenmgo kubwa la mradi huo ni kuzisaidia nchi hizo kukabiliana na hali ya jangwa inayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi na kujenga mneno katika matumizi ya ardhi kwa kupitia mkakati wa great Green Wall kwa ajili ya ukanda wa Sahara na Sahel . Damas Pod ni mratibu wa kitaifa wa mradi huo Burkina Fasso

(SAUTI YA DAMAS POD)

“Kipaumbele chetu ni kuirejesha ardi kubwa katika ubora wake na ndio maana FAO ilianzisha trekta la Delfino ili kutayarisha ardhi iliyomomonyoka kwa kutumia nyenzo muafaka. Kurejesha ubora wa ardhi ni mchakato na mradi ulichokifanya ni kuanzisha mchakato huu na unachotakiwa kufanya ni kufuatilia kwa takriban miaka  2 hadi 3 kabla ya mimea kuwa imara kuepuka meno ya wanyama.”

Ili kuchagiza kukua kwa mimea tena katika eneo hilolililogeuka jangwa mradi wa AAD unafanya utafiti wa mchango wa viumbe vilivyoko kwenye udongo kwa kufanya majaribio mbalimbali na teknolojia imedhihirisha kwamba bado hawajachelewa kubadili hali ya jngwa na kuwa ardhi nzuri inayoshamili mimea tena.

Watu 12500 kutoka vijiji 45 kupitia mradi huu sasa wamepata ujuzi kuhusu udhibiti endelevu wa ardhi. Saidou Sawadogo ni mkulima katika kijiji cha Miamanga

(SAUTI YA SAIDOU SAWADOGO)

“Hatua dhidi ya hali ya jangwa imetuwezesha kukusanya mawe na kujenga kingo zinazohitajika.”

Urejeshaji wa hali bora ya ardhi unafufua mfumo wa maisha na kuwaletea kipato wakati kupitia biashara mbalimbali kama ya mbao na ufugaji wa nyuki au utengenezaji wa mafuta na sabuni. Mfano huu wa Burkina Faso Fao inasema unadhihirisha kwamba dunia inaweza kukabiliana na hali ya jangwa na matunda kuonekana.