Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nataka kufanikiwa ili nisaidie wazazi wangu na nchi yangu:Mtoto Adama

Mtoto akiwa ameketi dawatini katika shule ya msingi mjini Doula, Cameroon  inayopatiwa ufadhili na UNICEF
© UNICEF/Tanya Bindra
Mtoto akiwa ameketi dawatini katika shule ya msingi mjini Doula, Cameroon inayopatiwa ufadhili na UNICEF

Nataka kufanikiwa ili nisaidie wazazi wangu na nchi yangu:Mtoto Adama

Amani na Usalama

Kutana na mtoto Adama mwenye umri wa miaka 12 kutoka Burkina Fasso , licha ya vita na machafuko yaliyokatili Maisha ya watu na kuwafanya maelfu ya watoto kutopata elimu nchini humo hajakata tamaa. Kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF anaenda shule sasa na ana ndoto ya kuwasaidia wazazi wake na nchi yake siku moja

Hii ni moja ya shule kwenye jimbo la Sahel nchini Burkina Fasso , jimbo ambalo usalama wake uko mashakani na kufanya kuwa vigumu kwa watoto kuhudhuria masomo. Lakini Adama na wenzie wako darasani , asante kwa msaada wa UNICEF na leo wanapewa somo la jinsi ya kujiandaa na kujilinda endapo shambulio la mtutu wa bunduki litatokea shuleni. Adama anasema

(SAUTI YA ADAMA)

“Hata kama hakujakuwepo na milio ya bunduki, punde tu tunaposikia firimbi tunatakiwa kufunga madirisha na kulala chini au kujificha chini ya madawati au viti.”

zaidi ya shule 1700 nchini Burkina Fasso zimelazimika kufungwa kwa sababu ya ongezeko la machafuko ya silaha na usalama mdogo ikiwemo shule ya kijijini kwa Adama.

(SAUTI YA ADAMA )

"Majambazi walikuja shuleni Kwetu. Walichoma vitabu vya shule yetu na makaratasi na kuwafukuza walimu. Walimuua baba wa mmoja wa rafiki zangu.”
Adama aliamua kuhamia mjini Dori kwenda kuishi na kaka yake ili aweze kuendelea na masomo kwani kijijini hali ilikuwa mbaya  sana

(SAUTI YA ADAMA )

“Ninapotafakari yote haya najihisi vibaya sababu siwezi tena kucheza na rafiki zangu. Tangu nije Dori sijaweza kuzungumza nao. Mara nyingi kabla sijalala nafikiria matukio yote haya ambayo yameathiri Kijiji chetu.”

Hivi sasa shirika la UNICEF linashirikiana na mamlaka za vijiji na wadau wengine kuhakikisha kwamba licha ya tishio lililopo watoto wanaweza kuendelea kusoma katika mazingira salama.

Na Adama anasema ana ndoto ya siku moja kumaliza shule, kufanikiwa na kuwa mtu ambaye atawasaidia wazazi wake na nchi yake.