Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa ombi la ufadhili kwa ajili ya kukabiliana na surua DRC

Mhudumu wa afya akimchanja mtoto dhidi ya surua nchini Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo
WHO
Mhudumu wa afya akimchanja mtoto dhidi ya surua nchini Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo

WHO yatoa ombi la ufadhili kwa ajili ya kukabiliana na surua DRC

Afya

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limetoa ombi la ufadhili zaidi ili kukabiliana na janga kubwa la surua linaloshuhudiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

Ombi hilo limekuja wakati huu ambapo idadi ya waliokufa kutoka na surua imevuka watu 6,000.

Kutokana na  uongozi wa waziri wa afya nchini DRC, WHO, muungano wa chanjo ulimwenguni, GAVI na wadau wengine walitoa chanjo kwa zaidi ya watoto milioni 18 walio chini ya umri wa miaka mitano kote nchini mwaka 2019.

Corneille Bihura, ni afisa wa afya katika kituo cha, CCLK,“leo tunatoa chanjo kwa sababu watoto wengi wamekuwa na Syria. Wanaokuja wakiwa wagonjwa wanatibiwa bila malipo. Tunahudumia karibu watoto watatu hadi watano ambao wameambukizwa surau kila siku. Tuna dawa za kuwatibu.”

Hata hivyo, katika maeneo mengine, idadi ya waliopokea chanjo inasalia kuwa ndogo ikiwa ni asilimia 25 ya visa vya surua vilivyoripotiwa ni miongoni mwa watoto waliozidi umri wa miaka mitano ambao wako hatarini zaidi. Justine Safari ni mama wa watoto sita,“nilisikia kwamba surau inaua na ndio maana nilileta watoto wangu wachanjwe.”

Tangu mwanzo wa mwaka 2019, takriban watu 310,000 waliripotiwa kuwa na surua ambapo janga hilo linazidishwa na idadi ndogo ya watu kuchanjwa hususan katika jamii zilizo hatarini, utapiamlo, miundo dhaifu ya afya, mlipuko wa magonjwa mengine na ugumu wa kufikia jamii zilizo hatarini na huduma ya afya kwa sababu za kiusalama, Gadafi Mundeke, ni mzazi, “hakuna mtu aliyeko katika jamii ambaye anapinga chanjo, hakuna, Chanjo hii ni muhimu sana kwetu.”

Desemba 2019, WHO ilitoa mafunzo kwa wauguzi 60 kutoka wizara ya afya kwa ajili ya kuendesha program ya ushirika wa jamii, elimu ya afya na ufuatiliaji ambapo wauguzi hao wanasaidia katika kukabiliana na hali ya sasa.