Je umeshawahi kuonja majani ya moringa yaliyopikwa kwa nazi? Basi kutana na mpishi kutoka Sri Lanka:IFAD

6 Januari 2020

Mabadiliko ya tabianchi yanayoikumba dunia hivi sasa yamewafanya watu wengi kutafuta kila njia ya kuyakabili au kupata suluhu mbadala. Mojawapo ni kutumia mapishi ambapo mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD unasema yanaleta mapinduzi kwa jamii nyingi ikiwemo nchini Sri Lanka ambako majani ya mti wa Moringa unaohimili ukame imegeuka mboga maridadi nma yenye lishe bora. 

Mti wa Moringa nchini Sri Lanka umepatiwa majina kemkem ikiwemo mti wa miujuza na rafiki kipenzi cha mama , mti ambao majani yake sasa ni chakula maarufu kote duniani yakiwa na lishe bora ambayo inabadili maisha ya wakulima wa vijijini nchini Sri Lanka.

Mpishi maarufu wa Italia Rubio ambaye hamasa yake ya kujifunza kuhusu vyakula mbalimbali imempeleka kila kona ya dunia leo yuko Sri Lanka kwenye shamba la Moringa la mmiliki na mkulima Hemamalika au mpishi Hema.

(SAUTI YA MPISHI RUBIO)

"Moringa ni mti wa kushangaza wenye faida nyingi. Mbali ya kuwa ni mti wenye virutubisho vingi na madini ya chuma , unasaidia sana kujenga kinga ya mwili na kuongeza damu.”

Hema amemualika mpishi Rubio jikoni kwake kutayarisha mboga ya Moringa Malluma inayopikwa kwa nazi, pilipili , limao  na majani mengi ya moringa. Baada ya kutia majani ya Moringa na pilipili , mpishi anaongeza vitunguu, vitunguu swaumu, binzari  chumzi na nazi. Na kisha anakaanga kwa dakika mbili hadi tatu anamalizia na ndimu, mboga tayari.

Akipika pia amemuelezea Rubio mafanikio yake na moringa na jinsi unavyohimili ukame na kuwa muhimu sana katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo inakabiliwa na mabadiliko ya tabianchi.

Ukame uliotawala unamaanisha wakulima ni lazima wabadili mwelekeo kwa mazao mapya na kujifunza kuwa na mnepo

(SAUTI YA HEMAMALIKA WIJERATNA)

“Kwa kuwa hili ni eneo kame , Moringa unakuwa vizuri hapa , wakati mwingine mtu unakuwa kwa miaka 10 hadi 15 na kama majani yanachumwa kila wakati basi mti unashamiri zaidi, kwa sababu ya ukame mti huu unatusaidia sana."

Hema alijifunza ,binu zote hizi kupitia program ya ushirika wa wakulima wafanyabiashara ambayo ni mradi unaofadhiliwa na IFAD na umewafaidisha zaidi ya wakulima wadogowadogo 50,000.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud