Kuna visa vipya 29 vya Ebola DRC tangu Desemba 18-31:WHO

3 Januari 2020

Shirika la afya ulimwenguni WHO leo limethibitisha kuwepo kwa visa vipya vya Ebola 29 kati ya Desemba 18 hadi 31 mwaka 2018. Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa leo na shirika hilo visa hivyo vimethibitishwa katika maeneo manane yenye vituo vinne vya afya vinavyotibu Ebola kwenye jimbo la Kivu ya Kaskazini.

Taarifa hiyo ya WHO inasema kati ya visa hivyo 29 visa 18 vimethibitishwa kwenye eneo la Mabalako, visa 4 Butembo, visa 5 Kalunguta, na visa 2 Katwa.

Visa vitatu kati ya visa vinne vilivyoripotiwa Butembo katika siku 14 zilizopita  vinahusishwa na mnyororo wa maambukizi ya watu zaidi ya 50 ambao ulianzia katika eneo la Aloya kwenye kituo cha afya cha Mabalako.

Mtu mmoja ambaye alieelezwa kupata Ebola kwa mara nyingine aliambukiza watu kadhaa wa familia yake. Na WHO inasema kuanzia Desemba 11 hadi 31 visa vipya vya Ebola vilivyothibitishwa vimefikia 40 kutoka katika maeneo 10 kwenye jimbo la Kivu Kaskazini.

Na mpaka kufikia tarehe 31 Desemba 2018 jumla ya visa vyote vya Ebola nchini DRC ni 3380 vikiwemo vilivyothibitishwa 3262 na vinavyokisiwa 118, huku jumla ya watu 2232 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter