Doria ya pamoja ya MINUSCA na polisi yadumisha usalama Ubangi CAR

2 Januari 2020

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, doria inayofanywa kwa ushirikiano wa jeshi la polisi la nchi hiyo, polisi wa Umoja wa Mataifa UNPOL wanaohudumu katika mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo ujulikanao kama MINUSCA inasaidia kuweka utulivu na kukabiliana na uhalifu.

Katika kivuko cha mto Ubangi polisi wa Umoja wa Mataifa UNPOL na wa serikali ya CAR wanaonekana wakiwa pamoja kwenye doria kwa lengo moja la kuhakikisha kuna uwepo wa polisi katika eneo hilo ili kukabiliana na uhalifu na uhamiaji haramu.

Outtara Moussa kutoka polisi wa MINUSCA anafafanua zaidi,“tunapokuwa kwenye mto, tunaenda kwenye vituo mbalimbali vya kutokea. Wadau wa polisi wanachunguza chini ya msaada wetu hati za kusafiria, hati ambazo zinaidhinisha Maboti haya kuzunguka kwenye mto. Pia tunaangalia ikiwa kuna wasafirishaji haramu. "

Wadau wa polis indio wanaodhibiti safari za boti mtoni pia wanaingilia kusaidia wale wanaokumbwa na dharura kama vile kuzama majini. Na polisi kwa upande mwingine wanajihusisha zaidi na masuala ya uhamiaji, wanaoingia na kutoka. Kama anavyosema Ouatarra pia hupata fununu za matukio ya uhalifu,“kwa upande mwingine wa mto, mara nyingi tunapata tarifa kwamba kuna wasafirishaji haramu wa mihadarati, kwa kupiga doroa mtoni inaruhusu kikosi cha wanamaji kuingilia kati boti za wanaume hao wanaosafirisha bangi.”

Timu hiyo ya mchanganyiko wa vikosi vya usalama vya CAR na polisi wa MINUSCA pia inafanya doria za watembea kwa miguu kandoni mwa mto Ubangi na kuwaelimisha watumiaji wa mto na daraja kuu la Ubangi kuhusu usalama wao.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud