Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kliniki ya bure ya Shamlapur yatoa matumaini mapya kwa wakimbizi wa Rohingya na wenyeji wao:UNHCR

Wanawake wakiwa wamelazwa hospitalini
UNFPA/Ollivier Girard
Wanawake wakiwa wamelazwa hospitalini

Kliniki ya bure ya Shamlapur yatoa matumaini mapya kwa wakimbizi wa Rohingya na wenyeji wao:UNHCR

Afya

Klinini ya mazoezi ya viungo inayotoa huduma bure kwa wakimbizi wa Rohingya na jamii zinazowahifadhi nchini Bangladesh imeleta matumaini mapya  kwa pande zote zinazopokea huduma . 

Katika kliniki hii ya Shamlapur nchini Bangladesh huduma inayotolewa si ya vioungo pekee bali pia tiba ya maumivu ya mgongo na maradhi mengine kama ugonjwa wa kutetemeka au kukakamaa.

Ilianzishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR mwezi Julai mwaka 2018 kwa lengo la kuwasaidia wakimbizi wa Rohingya na jamii zinazowahifadhi katika eneo ambalo limepokea wimbi kubwa la wakimbizi.

Kliniki hii ina madaktari wawili wataalamu wa mazoezi ya viungo na wasaidizi wawili na wote wanafanya kazi bure bila malipo yoyote. Huduma wanayotoa ni mpya kabisa katika eneo hili na watu zaidi ya 1000 wameshafaidika na matibabu tangu ilipofungiliwa hadi kufikia Oktoba mwaka huu wa 2019. Hazera mwenye miaka 55 mkimbizi wa Rohingya ni miongoni mwa wagonjwa katika kliniki hii anasema

Nitakapopona kwa mapenzi ya Mola, nitakwenda msikitini  na nitapika nyama na kuwapa chakula watoto.”

Na mmoja wa wataalam wanaomuhudumia ni Naushini Anjun

"Kituo hiki cha mazoezi ya viungo ni cha muhimu sana kwa sababu ndio kituo pekee  na cha aina yake kwenye eneo hili, na mara nyingi tunatumia tiba ya mazoezi ya kawaida ya asili lakini pia tunayo mazoezi ya umeme na mbali ya hapo tuna chumba cha mazoezi chenye vifaa, tuna vifaa vya kutosha mahitaji ya wagonjwa wetu wote. Wengi wa wagonjwa wetu wanamatatizo ya mgongo au kupooza au maumivu ya magoti ,wote Warohingya na jamii zinazowahifadhi na kutoa huduma kwa makundi yote inatufanya tujihisi vizuri.”

Mzee Golam Kibria ana umri wa miaka 100 ni raia wa Bangladesh yeye huja katika kliniki hii mara kwa mara

Warohingya wamefanya hapa kuwa makazi yao ya muda, na wanatengeneza maisha yao hapa, nahisi vizuri sana kuhusu hilo. Waislam watakuja kuwasaidia waislam wenzao.”

Miradi ya kusaidia wakimbizi na jamii zinazowahifadhi kama huu ni miongoni mwa ajenda iliyotawala kongamano la kimataifa la wakimbizi lililokunja janvi Geneva wiki iliyopita.