Kiswahili kinazidi kutamba hata vyuoni ikiwemo Chuo Kikuu cha Nairobi Kenya

27 Disemba 2019

Wigo wa lugha ya Kiswahili unaendelea kupanuka kila uchao na ni kwa mantiki hiyo ambapo watu wengi wanajikuta wakichukua masomo ambayo yanajikita pia na lugha hiyo.

Mapema mwezi huu nimepata fursa ya kutembelea Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya ili kufahamu mengi zaidi kuhusu kitengo cha tafsiri na ukalimani ambacho tunashirikiana nacho katika kutafsiri baadhi ya kurasa za kazi za Umoja wa Mataifa ambazo utaweza kuzipata kwenye wavuti wetu kupitia news.un.org/sw. Nimezungumza na mhadhiri wao ambaye amenidokezea kuhusu kitengo hicho
(Play clip)

Lakini je wanafunzi wenyewe wanasema nini? tumsikie kwanza Rajab Abdalla kutoka Tanzania ambaye anasomea utafsiri ukijumuisha lugha ya Kiswahili nchini Kenya, kulikoni?

(Play clip)

Kwa upande wake kijana Mary Mukami anatoa ushauri kwa vijana katika mtazamo wao kuhusu Kiswahili

(Play Clip)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter