Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu ya kifo dhidi ya wauaji wa Khashoggi ni zahma juu ya zahma:Callamard

Agnes Callamard
UN Photo.
Agnes Callamard

Hukumu ya kifo dhidi ya wauaji wa Khashoggi ni zahma juu ya zahma:Callamard

Haki za binadamu

Mtaalam maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji na mauaji ya kiholela Agnes Callamard amesema ameshtushwa sana na hukumu ya kifo waliyopewa wanaodaiwa kumuua mwandishi wa Habari wa Saudia Jamal Khashoggi huku walioamuru mauaji hayo wakiachwa bila kuguswa.

Bi. Callamard amesema amepigwa na mshituko mara mbili baada ya watu watano kuhukumiwa kifo juma hili kwa mauaji ya Khashoggi kufuatia kesi iliyoendeshwa kwa siri.

”Wauaji walikutwa na hatia na kukatiwa hukumu ya kifo. Nikipinga hukumu ya kifo huu ni mshituko wa kwanza kwangu. Hata hivyo wale walioamuru mauaji hayoa sio tu kwamba wameachwa huru lakini hawakuguswa kabisa na uchunguzi wala kesi, huu ni mshituko wa pili kwangu, huu ni ukiukaji wa haki na dharau isoyokubalika kwa waathirika.”

 Ameongeza kuwa chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu kifo cha Khashoggi yalikuwa ni mauaji ambayo ufal;me wa Saudi Arabia unapaswa kuwajibishwa. “Kesi hii inahitaji uchunguzi katika mnyororo wa maamuzi, ili kubaini muandaaji, pamoja na waliochochea, walioruhusu au kufumbia macho mauaji hayo kama vile mwana mfalme” ameongeza mtaalam huyo.

Callamard amesisitiza kwamba hakuna wakati wowote katika kesi hiyo uliofikiria wajibu wa serikali .”Maafisa 18 wa Saudia waliokuwepo wenyewe kwenye ubalozi wa saudia mjini Instanbul kwa zaidi ya siku 10 walisafisha eneo la uhalifu. “Huu ni uingiliaji wa haki na ukiukwaji wa mkataba wa Minnesota kwa ajili ya uchunguzi wa mauaji ya kupangwa. "Kuwepo kwa daktari wa uchunguzi aliyejiorodhesha katika timu rasmi ya mauaji angalau saa 24 kabla ya uhalifu huo, na kujadili kumuondoa Bwana. Khashoggi saa mbili kabla ya kutokea kwa mauaji yake, pia inaonyesha wazi kuwa mauaji yalipangwa."

Callamard amesema jaji anaonekana kuhitimisha kwamba mauaji ya  Bwana. Khashoggiilikuwa ni ajali kwa kuwa inaonekama hakukuwa na dhamira , lakini bado amewahukumu washitakiwa kifo katika ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa za haki za binadamu. Hukumu ya kifo itolewe tu ambapo mazingira ya kesi yalifuata haki moja wapo ni katika mauaji ya kimataifa”

Mtaalam huyo pia amekosoa mwenendo wa usikilizaji wa kesi hiyo ambao ulifanyika kwa faragha . Callamard pia amesema watuhumiwa walirejelea kusema mara kadhaa wakati wa kesi kwamba walikuwa wanatekeleza amri na mwendesha mashitaka alisema hadharani kwamba Saud al-Qahtani, mshauri binafsi wa mwana mfalme alitaka kutekwa kwa bwana Khashoggi kwa madai kwamba alikuwa tishio la usalama wa taifa.

Hata hivyo mshauri huyo hakushitakiwa kwa lolote na yuko huru Na balozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul Mohammad al-Otaibi, aliyeruhusu ofisi ya ubalozi wake kuwa sehemu ya uhalifu hakukutwa na hatia yoyote.

Mwezi Juni 2019, Callmard alitoa ripoti kufuatia uchunguzi wa miezi sita  wa mauaji ya Khashoggi yaliyofanyika 2028. Ripoti hiyo ilitathimini Ushahidi kwa misingi ya sheria za kimataifa za haki za binadamu na kufikiria hatua za kuchukuliwa ambazo zingezuia mauaji hayo.