Guterres alaani shambulio la Jumanne Soum, Burkina Faso

Burkina Faso imekuwa mlengwa wa mashambulizi tangu 2015.
WFP/Simon Pierre Diouf
Burkina Faso imekuwa mlengwa wa mashambulizi tangu 2015.

Guterres alaani shambulio la Jumanne Soum, Burkina Faso

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amelaani vikali shambulio lililotekelezwa Jumanne na kikundi cha watu waliokuwa wamejihami wasiojulikana huko kaskazini mwa Burkina Faso.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu Jumatano, Bwana Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwatakia afueni ya haraka majeruhi wa shambulio lililofanyika Arbinda jimbo la Soum.

Katibu Mkuu huyo pia ameelezea mshikamano wa Umoja wa Mataifa kwa serikali na watu wa taifa hilo la Afrika magharibi.

Bwana Guterres amekumbusha utayari wa Umoja wa Mataifa kuendelea kusaidia serikali ya Burkina Faso n anchi zingine za ukanda wa Sahel katika juhudi zao za kukabiliana na ugaidi na ukatili uliokithiri

Kwa mujibu wa duru za habari, kundi la waislamu wenye msiamo mkali waliuwa makumi ya raia, wengi wakiwa ni wanawake katika shambulio hilo lililochukua saa kadhaa.