Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres aelezea kusikitishwa na mauaji ya raia Nigeria, atuma salamu za rambirambi kwa familia

Raia wa  Nigeria waliokimbia Cameroon kutokana na machafuko ya Boko Haram
UN Photo/Eskinder Debebe)
Raia wa Nigeria waliokimbia Cameroon kutokana na machafuko ya Boko Haram

Guterres aelezea kusikitishwa na mauaji ya raia Nigeria, atuma salamu za rambirambi kwa familia

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameelezea kusikitishwa na ripoti za raia kuuwawa na wengine kutekwa na kundi la watu waliojihami kaskazini mwa jimbo la Borno kwenye eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Katibu Mkuu kupitia taarifa yake iliyotolewa na msemaji wake Jumanne jijini New York Marekani ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya wahanga na kurejelea mshikamano wa Umoja wa Mataifa na watu na serikali ya Nigeria.

Katibu Mkuu amekumbusha kwamba mashambulio ya makundi yaliyojihami kwenye mzozo yanayolenga raia, wahudumu wa misaada ya kibinadamu na miundombinu ya raia yanakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu.

Taarifa ya Katibu Mkuu imemnukuu akisema kwamba watekelezaji wa uhalifu huo ni lazima wawajibishwe na kwamba sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na sheria ya kimataifa ya kibinadamu ni lazima ziheshimiwe kikamilifu na raia wote wa Nigeria ni lazima walindwe.