Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi tatu za Afrika zazuia milipuko ya ugonjwa wa polio-WHO

Mhudumu wa afya aktioa chanjo ya polio kwa mtoto Kaloko, Ndola, Zambia.
© UNICEF/Karin Schermbrucke
Mhudumu wa afya aktioa chanjo ya polio kwa mtoto Kaloko, Ndola, Zambia.

Nchi tatu za Afrika zazuia milipuko ya ugonjwa wa polio-WHO

Afya

Kenya, Musumbiji na Niger wamezuia milipuko ya ugonjwa wa polio ambayo ilishuhudiwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi 24 iliyopita na kuchangia nchi hizo kutangazwa kuwa zisizokuwa na ugonjwa wa polio kwa mujibu la tangazo la shirika la afya duniani WHO lililotolewa leo.

Kwa mujibu wa WHO ugonjwa huo wa polio utokanao kusambaa kwa kinyesi cha waliopatiwa chanjo kwenda kwa wasio na ikinga uligunduliwa katika nchi tatu mwaka 2018 na mapema mwaka 2019 na uliwaathiri  jumala ya watoto 14.

Kumaliza kwa milipuko katika nchi hizi tatu ni thibitisho kuwa shughuli za kupambana na polio na matumizi ya chanjo ya hali ya juu inaweza kuzima milipuko iliyobaki eneo hilo. Amesema Dr Modjirom Ndoutabe mratibu wa kundi la WHO la kupambana na polio eneo la Afrika.

Visa vya virusi vya polio vinavyotokana na chanjo ni vichache lakini huwaathiri watato ambao hawajachanjwa na waliopata chanjo kidogo.

Wakati watoto wanapochanjwa, chanjo hiyo hubaki kwenye matumbo yao kwa kipindi kifupi kuwapa kinga wanayohitajia na kisha hutoka kwa njia ya haja kubwa ambapo inaweza kubaki katika mazingira.

Ikiwa utoaji chanjo katika jamii na usafi unabaki kuwa duni virusi vilivyo katika mazingira vinaweza kuwaambukiza watu wasiojua.

Kumaliza milipuko huo huduma kwenye nchi zilizoathirika, makundi ya uchunguzi na mahabara ni lazima yathitbitishe kuwa hakuna maambukizi ya polio yanayotambuliwa kutoka kwa sampuli zinazokusanywa kutoka kwa watoto waliopooza kwa kipindi cha karibu miezi tisa.

Nchi ambazo bado zinashushua milipuko ya ugonjwa wa polio ni pomoja na Angola, Benin, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Côte d'Ivoire, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Ethiopia, Ghana, Nigeria, Togo na Zambia.

Kati ya masuala yanayochangia kushuhudiwa milipuko hiyo ni udhaifu katika utoaji chanjo, watu kukataa chanjo, vigumu kuyafikia maeneo mengine, kampeni chache za utoaji chanjo ambazo hufanya vigumu kuwafikia watoto.