Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ecuador komesheni ubaguzi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika-UN

Mji wa Quito, Ecuador
UN/Rocío Franco
Mji wa Quito, Ecuador

Ecuador komesheni ubaguzi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika-UN

Haki za binadamu

Serikali ya Ecuador imetakiwa kuongeza juhudi zake ili kuhakikisha sheria inafuatwa na kutekeleza mipango ya kukomesha ubaguzi wa rangi unaowakabilia Raia weusi wa Ecuador na watu wenye asili ya Afrika.

Wito huo umetolewa leo na kundi la wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa mjini Quito baada ya kuhitimisha ziara yao nchini humo.

Ahmed Reid mwenyekiti wa jopo la wataalamu wa kundi hilo linalohusika na watu wenye asili ya Afrika akiwasilisha tarifa baada ya ziara yao amesema “Watu hao wanateseka sana hususani katika kupata fursa za haki, usalama, ardhi, maji safi, elimu, huduma za afya, nyumba na fursa za kiuchumi.”

Ameongeza kuwa ni asilimia 7.2 tu ya watu wote wa Ecuador ndio wenye asili ya Afrika lakini ndio asilimia 40 ya wale wanaoishi katika umasikini. “Ecuador ni lazima itekeleze na kuhakikisha sheria na será za kulinda haki za watu hawa na kukomesha ubaguzi, kuwatenga na madhila ya ufukara unnaowakabili.”

Kundi hilo la wataalam limeweka msisitizo zaidi katika jimbo la Esmeraldas ambako karibu asilimia 70 ya watu wote wana asili la Afrika.” Esmeraldas ni moja ya majimbo masikini kabisa Ecuador, asilimia 85 ya watu wanaishi chini ya kiwango cha umasikini, asilimia 23 penkee nsii wenye firsa ya baadhi ya huduma za msingi huku asilimia 15 ya watu wote hawajui kusoma wala kuandika.” Amesema bwana Reid na kuongeza kuwa kundi la wataalam hao linakaribisha miradi ya kitaifa ya serikali kukabiliana na ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa aina zingine, chuki dhidi ya wageni na hali ya kutovumiliana inayowakabili raia wa Ecuado wenye asili ya Afrika lakini ni dhahiri kwamba bado kuna kibarua kikubwa ili kukomesha kiwango kikubwa cha ubaguzi na umasikini kwa watu hawa.

Wataalam hao wamesema “watu wenye asili ya Afrika pia wanakabiliwa na ubaguzi wa kimazingira mara kadhaa maji na mazingira yao yakichafuliwa, jamii zao zikipewa vitisho na hakuna hatua za kutosha zinazochukuliwa na serikali.

Wataalam wamesisitiza kuwa serikali haipaswi kuwa tofauti linapokuja suala la ukiukwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji unaofanywa na viwanda na makampuni. Ni lazima ikomeshe ukwepaji wa sheria kwa masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu na ubaguzi wa kimazingira.

Wakati wa ziara yao kuanzia 16 hadi 20 Desemba walifanikiwa kuzuru Quito, San Lorenzo na Esmeraldas na ripoti yao kamili na mapendekezo itawasilishwa kwenye baraza la haki za binadamu Septemba 2020.