MONUSCO kuendelea DRC kwa mwaka mwingine mmoja:UN

20 Disemba 2019

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio kuongeza muda wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC (MONUSCO) ambao ulikuwa unamalizika leo Desemba 20.

Azimio hilo linaanza kuchukua hatua kuelekea hatimaye kufungwa kwa mpango wa MONUSCO na limetoa ombi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufanyakazi na serikali ili kuunda mkakati wa kuondoka utaokaojikita na mafanikio yaliyopatikana ambao utapendekezwa kwenye Baraza la Usalama sio Zaidi ya tarehe 20 Oktoba 2020.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe watatu wa afrika kwenye Baraza la Usalama , balozi wa afrika ya Kusini kwenye Umoja wa Mataifa Xolisa Mabhongo amekaribisha mpango huo na kusema “ni muhimu kwamba kuondoka kwa MONUSCO kuwe ni kutokana na mabadiliko chanya ya hali nchini humo na kutimiza azma ya mpango huo”

Kwa upande wake mwakilishi wa DRC Paul Empole Lokoso Elambe amesema “Wazo la kukita vikosi vya MONUSCO katika majimbo sita ambako inaonekana kuwepo kwa vikosi ni muhimu  na lazima linaenda sanjari na ombi la serikali ya nchi yake la kutaka vikosi view zaidi katika majimbo hayo ambako kiwango cha vitisho kiko juu na kupunguza uwepo wa vikosi katika nmaeneo ambako vitisho sio vikubwa tena.”

Ameongeza kuwa “Rais Felix Tshisekedi ametoa wito wa kufanyia mabadiliko MONUSCO ambao unapendekeza kupunguza vikosi ambavyo vitatakiwa kuwa vichache lakini bora Zaidi vikiwa na vifaa vyote vya kivita.”

Azimio hilo pamoja na kuongeza mkataba wa MONUSCO hadi Desemba mwakani linasisitiza vipaumbele viwili vikubwa kwa MONUSCo ambavyo ni “kulinda raia na kusaidia kurejesha utulivu na kuimarisha taasisi za serikali ya DRC.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter