Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yampongeza Papa Francis kwa juhudi zake za kuleta amani duniani na kuwatetea wanyonge

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kushoto) alipokutana na Papa Francis mjini Vatican Roma 20 Desemba 2019
UN Photo/Rein Skullerud
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kushoto) alipokutana na Papa Francis mjini Vatican Roma 20 Desemba 2019

UN yampongeza Papa Francis kwa juhudi zake za kuleta amani duniani na kuwatetea wanyonge

Amani na Usalama

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amempongeza kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis kwa kupunguza madhila kwa watu na kutetea hadhi ya haki za binadamu. 

Akizungumza baada ya mkutano wao mjini Roma Italia , Katibu Mkuu amesema kuwa Papa Francis amekuwa katika mstari wa mbele kuzungumzia hatma za wale wanaokumbwa na matatizo wakiwemo wakimbizi na wahamiaji, kwa kuukabili umaskini na kutokuwepo usawa na kuitisha kujengwa mahusiano mema kati ya jamii na mambo mengine.

Guterres ameongeza kuwa Papa amekuwa muungaji mkono mkubwa wa kazi ya Umoja wa Mataifa, ikiwemo safari aliyoifanya katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwaka 2015 wakati dunia ilifikia makubaliano kuhushu maendeleo endelevu.

Guterres alisema kuwa mkutano wao una umuhimu hasa wakati huu wa msimu wa sherehe za krismasi akielezea kuhusunishwa na changamoto zinakumba jamii za wakiristo ambazo kwa sasa haziwezi kusherehekea krismasi kwa amani. Na kuongeza kuwa, "atika wakati huu wa misukosuko na majaribu , tunapaswa kushikamana kwa pampja kwa amani na utulivu, na ndio ari ya msimu hu una hii iwe katika maono , muongozo na mfano. Nakushukuru sana papa na nawatakia kila la heri wote wanaosherehekea  amani kwa ajili ya Chrismas na mwaka mpya wenye baraka.”

Naye Papa mtakatifu Francis akihimiza kuhusu mshikamano huo na kuilinda dunia ambayo ndio maskani yetu amesema, “hebu tujitambue kwamba sote ni wajumbe wa ubinadamu mmoja na tuitunze dunia yetu ambayo imerithishwa kizazi hata kizazi na Mungu, kwa sababu tunalima na kuwaachia watoto wetu kama urithi. Ahadi ya kupunguza hewa chafuzi na kuenzi mfumo wa maisha ni suala la dharura na la lazima. Hebu na tuchue hatua kabla hatujachelewa

Na kuhusu ukatili na chuki zinazoendelea duniani Katibu Mkuu Guterres amesema ni jambo la kuvunja moyo kuona wayahudi wakiuawa kwenye masinagogi  na makaburi yao yakiharibiwa, waislamu wakiuawa misikitini na maeneo yao ya ibada yakiharibiwa huku wakiristo wakiuawa na makanisa yao kuteketezwa.

Katibu mkuu pia amesema kuwa mengi yanahitaji kufanya ili kuleta uelewano na kukabiliana na chuki.

Guterres amesema Umoja wa Mataifa umezindua mpangowa kulinda maeneo matakatifu na kuweka mikakati ya kukabiliana na uchochezi.