Nchi lazima zilipe kipaumbele suala la haki za binadamu katika sera za uhamiaji: UN

17 Disemba 2019

Nchi zinastahili kuzipa haki za binadamua umuhimu katika sera zao na mijadala inayohusu uhamiaji na kuchukua hatua za kumaliza kauli za uchochezi, kwa mujibu wa wataalamu wa haki za binadamu wa umoja wa Mataifa  kwenye ujumbe wao kuelekea siku ya uhamiaji duniani tarehe 18 Desemba.

Masuala ya usalama yanatumiwa kwa njia isiyofaa kuwaona wahamiaji kuwa wahalifu na pia watu wanaojaribu kuwasaidia, amesema Felipe González Morales ambaye ni mtaalam maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu kwa wahamiaji.

Katika kipindi muhimu ambapo sera za uhamiaji zinaangaliwa upya katika sehemu  mbalimbali na nchi, ni muhumu masuala ya usalama yasichukue nafasi ya haki za wahamiaji, wataalamu hao wamesema.

Kulinda haki za binadamu za kila mmoja inastahili kubaki kitovu ndani ya sera zote za nchi.

Wataalamu hao pia wamezitaka nchi kuchukua hatua zaidi kuzuia kauli za chuki na uchochezi dhidi ya wahamiaji.

Kauli za uchochezi huleta unyanyapaa na kusababisa wahamiaji kuonekana kama wahalifu, hali ambayo huathiri haki zao za binadamu, ni wakati nchi zinastahili kuchukua hatua kupambana na hili hii, wataalamu hao wamesema.

Wataalamu hao wameongeza kuwa kuibuka suala la wakimbizi duniani kumetoa fursa ya kuhakikisha kuwa haki za wanawake , wanaume , wasichana na wavulana zimeheshimiwa katika hatua zote za uhamiaji.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud