Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nimejifunza kwamba kukirimu wakimbizi sio lazima uwe tajiri:Guterres

Kongamano la kwanza la kimataifa la wakimbizi linaendelea mjini Geneva Uswis 17 Desemba 2019
©UNHCR/Mark Henley
Kongamano la kwanza la kimataifa la wakimbizi linaendelea mjini Geneva Uswis 17 Desemba 2019

Nimejifunza kwamba kukirimu wakimbizi sio lazima uwe tajiri:Guterres

Msaada wa Kibinadamu

Tatizo la wakimbizi ni jukumu la kila mtu sio wakimbizi au nchi zinazowahifadhi pekee, kwani nimejifunza ukarimu sio lazima uendane na utajiri. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hii leo katika kongamano la kimatifa kwa ajili ya wakimbizi linaloendelea mjini Geneva Uswis.  

Antonio Guterres amesistiza kwamba dunia ina deni kwa nchi zote na jamii zinazokaribisha idadi kubwa ya wakimbizi na deni hilo ni la shukrani. Hata hivyo amesema “lakini shukran pekee haitoshi, katika wakati huu wa msukosuko, jumuiya ya kimataifa lazima iongeze jitihada za kusaidia jukumu hili kwa pamoja. Muktadha wa ulimwengu unaweza kuonekana kuwa unakataza. Mgawanyiko na ushindani  kote duniani vinachangia hali isiyotabirika na ukosefu wa usalama huku shida ya mabadiliko ya tabianchi inaongeza zahma. Wengi katika jamii zetu wanahisi wametengwa na kuachwa nyuma.”

Kattibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la kimataifa la wakimbizi mjini Geneva Uswis
©UNHCR/Pierre Albouy
Kattibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la kimataifa la wakimbizi mjini Geneva Uswis

Guterres amesema kuwaachia mzigo wa wakimbizi watu wachache kwani kuwakirimu wakimbizi sio lazima uwe tajiri ni moyo wa kufungua mlango na kusaidia“sasa kuliko wakati mwingine wowote tunahitaji ushirikiano wa kimataifa utendaji na hatua zinazofanya kazi. Na hi indio sababu tuko hapa. Tunahitaji majibu mazuri kwa wale wanaokimbia na msaada botara kwa jamii  na nchi ambazo zinawapokea na kuwahifadhi”.

Ameongeza kuwa zaidi ya watu milioni 70 wamelazimika kukimbia makwao, wakiwemo wakimbizi milioni 25. Na shirika la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR likitaja idadi hiyo kuwa ni kubwa zaidi katika historia.

Na amesema cha kustaajabisha ni kwamba nchi zinazoendelea na za kipato cha wastani ndiyo zinazobeba mzigo mkubwa wa wakimbizi na ziko tayari kusaidia sio tu kwa masuala ya kibinadamu bali pia katika maendeleo na kwingineko "

Mipaka na milango imekuwa ikifungwa kwa wakimbizi ambapo hata watoto wakimbizi wamekuwa wakitenganishwa na familia zao, tunahitaji kusisitiza haki za binadamu za wakimbizi.”

Najla Umda Adam Suleiman alikimbia pamoja na familia yake na kwenda Chad akiwa na umri wa miaka mitatu tu baada ya vika kuzuka kwao kwenye jimbo la Darfur Sudan
© UNHCR/Modesta Ndubi
Najla Umda Adam Suleiman alikimbia pamoja na familia yake na kwenda Chad akiwa na umri wa miaka mitatu tu baada ya vika kuzuka kwao kwenye jimbo la Darfur Sudan

Na hivyo amesema kudumisha mkataba wa ulinzi kwa wakimbizi wa mwaka 1951 na mkataba wa karibuni wa kimataifa ndio muongozo.

Mkuu wa UNHCR atoa wito wa hatua madhubuti

Naye Kamishina mkuu wa wakimbizi Filippo Grandi akisistiza umuhimu wa kuwasaidia wakimbizi amesema “Umasikini, kutokuwepo haki na mabadiliko ya tabia nchi vinachopchea machafuko na watu kutawanywa huku migogoro ya muda mrefu ikionekana kukita mizizi.

Grandi amesisitiza kwamba “wakati ni sasa kwa kupiga jeki hatua zetu kwa wakimbizi, tunahitaji mtazamo thabiti kuchagiza na kuhusisha watu na taasisi zote katika jamii kuwanusuru wakimbizi kote duniani.”

Kamishna mkuu wa UNHCR Fillipo Grandi akizungumza na vyombo vya habari. (Picha kutoka maktaba)
Credit English (NAMS)
Kamishna mkuu wa UNHCR Fillipo Grandi akizungumza na vyombo vya habari. (Picha kutoka maktaba)

 

Kama mwejeji mwenza wa mkutano huo Kamishina mkuu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa Filippo Grandi ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza jitihada za msaada wake kwa watu wanaohitaji ulinzi.

Amesema “dunia iko katika mtikisiko mkubwa na wakimbizi milioni 25 wanatuangalia sisi kwa ajili ya suluhu za changamoto zao”

Akitathimini hatua za sasa za kimataifa kuhusu suala la wakimbizi kama ni ndogo na hazilingani bwana Grandi ameongeza kuwa “kukiwa na watu milioni 71 ambao wamekimbia makwao kote duniani wengine wakiwa wakimbizi wa ndani au nje ya nchi zao huu ni wakati wa kupiga jeki hatua zetu za kushugulikia suala hili.”

Amesema badala ya kuonyesha mshikamano kwa watu wenye mahitaji nchi zizlizo na rasilimali Zaidi zimewageuzia mzigo mataifa masikini kabisa. Na hii amesema “inamaanisha kwamba wakimbizi wanasukumwa kando na mara nyingi katika makambi, wakikatwa katika masuala ya kijamii na Maisha ya kiuchumi kwenye jamii zinazowahifadhi. Msaada wa kibinadamu unasaidia nab ado ni muhimu sana lakini hautoshelezi na unapelea kuweza kubadili mwelekeo kutoka kukata taa kuingia katika matumaini .”

Switzerland yaahidi dola milioni $125 kwa miaka minne ijayo

Akichagiza msaada kwa ajili ya kusaidiana kimataifa kubeba mzigo wa wakimbizi kansela wa Uswis Ignazio Cassis amesema nchi yake imejitolea ahadi ya dola milioni 125 katika miaka minne ijayo kwa ajili ya ulinzi kwa wakimbizi.

Ingawa karibu wakimbizi 8 kati ya 10 wanahifadhiwa katika nchi zinazoendelea miji ya Uswis imekuwa ikichangia kwa ulinzi wao kwa kusaidia kuwajumuisha tena katika jamii zao  amesisitiza bwana cassid kama mwenyeji mwenza wa mkutano huo .

Aya Mohammed Abdullah, mkimbizi wa zamani wa Iraq ambaye kwa sasa anaishi Uswis akihutubia kongamano la kimataifa la wakimbizi Uswis
©UNHCR/Mark Henley
Aya Mohammed Abdullah, mkimbizi wa zamani wa Iraq ambaye kwa sasa anaishi Uswis akihutubia kongamano la kimataifa la wakimbizi Uswis

“Maisha ni kama baiskeli unahitaji kusonga mbele kuepuka kupoteza uwiano, hii pia inatugusa sote hatupaswi kupoteza uwiano wet una kutazama mbele”. Ameongeza.

Na kwa niaba ya Ujerumani Heiko Maas waziri wa mambo ya nje ametoa wito wa mzigo wa wakimbizi kugawanywa miongoni mwa wanaojiweza na wenye fursa kubwa.

Pakistan: miaka 40 ya kuhifadhi wakimbizi

Akizungumzia shinikizo lililoko kwa matifa yanayoendelea yaliyoacha mipaka yake wazi kwa ajili ya familia zilizo hatarini zilizolazimika kukimbia makwao waziri mkuu wa Pakistan Imran Khan amesema kwamba wimbi hilo kubwa la wakimbizi linasababisha matatizo ambayo hayawezi kufikirika kwa mataifa Tajiri.

Ameongeza kuwa Ulaya imekuwa ikihaha kwa njia nyingine na wakimbizi ukizingatia kuibika kwa wanasiasa wenye kusaka sifa ambao wanafaidika na zahma za kijamii na kudhani kwamba wageni ni tishio katika jamii zao. Amesema Pakistan ambayo inahifadhi karibu wakimbizi milioni 3 ni nchi ambayo ina tatizo kubwa la ajira na tunatambua tunachokipitia.