Utipwatipwa na lishe duni ni mizigo miwili mikubwa ya afya kwa nchi masikini:WHO 

16 Disemba 2019

Zaidi ya nchi 1 kati ya 3 za kipato cha wastani na kipato cha chini zinakabiliwa na changamoto kubwa mbili za kiafya , utipwatiwa na lishe dunia kutokana na mabadiliko katika mifumo ya chakula imesema ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO iliyochapishwa leo kwenye jarida la kimataifa la afya The Lancet. 

 Kwa mujibu wa ripoti hiyo mtazamo mpya unahitajika kusaidia kupunguza matatizo hayo mawili ya utapiamlo kwa wakati mmoja utipwatipwa na lishe duni ambayo yanatokana na ongezeko la mabadiliko ya haraka ya mifumo ya chakula katika nchi nyingi. 

Na hii ni muhimu zaidi kwa kipato cha chini na cha wastani ambako zaidi ya theluthi moja ya nchi hizo zimekuwa na matatizo yote mawili ya utapiamlo nchi 45 kati ya 123 katika miaka ya 1990 na nchi 48 kati ya 126 katika miaka ya 2010 hususan AfrikaKusini mwa Jangwa la sahara, Asia Kusini,Asia Mashariki na Pasifiki.

Kwa mujibu wa Dkt. Francesco Branca kutoka idara ya lishe na maendeleo ya WHO ambaye ni mwandishi mkuu wa ripoti hiyo lishe duni na utipwatipwa vinaweza kusababisha athari ya kizazi hadi kizazi kwani athari wakati wa ujauzito zitaathiri watotowatakaoazaliwa pia,na kutokana na mabadiliko ya mifumo ya chakula watu wengi wamejikuta katika zahma zote mbili katikanyakati tofauti za maisha yao na kuongeza athari za kiafya.

Dkt. Branca anasema kuwa,  "tunakabiliwa na ukweli mpya wa lishe, hatuwezi tena kuziita nchi za kipato cha chini na zenye lishe duni au nchi za kipato cha juu na zinahofia tuu utipwatipwa.Mifumo yoteya utapiamlo ina chanzo ambacho ni mifumo ya chakula iliyoshindwa kuwapa watu wake lishe yenye siha, salama , ya gharama nafuu na endelevu. Kubadili hili kutahitaji hatua katikamifumoyote ya chakula kuanzia uzalishaji na usindikaji, kupitia biashara na usambazaji, bei, masoko, uwekaji chapa hadi matumizi na utupaji. Sera zote za muhimu na uwekezaji vinapaswa kutathminiwa upya.”

 Hali halisi

Kimataifa inakadiriwa kwamba takriban watu bilioni 2.3  watoto na watu wazima wana uzito wa kupindukia au utipwatipwa na zaidi ya watoto milioni 150 wamedumaa.

Hata hivyo katika nchi za kipato cha chini na cha wasttani matatizo haya yanayoibukia yanaingiliana kwa watu binafsi, familia, jamii na nchi. 

 Na ripoti hii mpya inatathimini mwenendo wa muingiliano huo uitwao mizigomwili ya utapiamlo pamoja pia na mabadiliko ya mifumo ya jamii na chakula ambayo inaweza kuchangia kutokea na athari zake na pia hatua za kisera ambazo zinaweza kusaidia kushughulikia mifumo yote ya utapiamlo.

Ripoti imetumia takwimu kutoka nchi za kipato cha chini na cha wastani za miaka ya 1990 na 2010 ili kubaini nchi gani ina mzigo mara mbili wa utapiamlo.

Nini cha kufanya

Ripoti inasema lishe bora inapunguza hatari ya mifumo yote ya utapiamlo kwa kuchagiza ukuaji wenye afya, maendeleo na kinga ya kuhimili magonjwa, kuzuia utipwatipwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NDCs) katika maisha.

Ripoti imeja vochochezivya afya bora kuwa ni pamoja na unyonyeshaji wa maziwa ya mama miaka miwili ya mwanzo wa maisha ya mtoto, ulaji wa matunda aina mbalimbali na mbogamboga, nafaka, jamii ya karanga na mbeguvitamini, kula kwa wastani vyakula vitokanavyo na wanyama, vinywaji vyenye sukari nyingi, mafuta na mafuta yasiyoyeyuka na chumvi.

Magonjwayanayoweza kusababishwa na lishe hiyo duni ni pamoja na maradhi ya moyo, kisukari aina ya 2, shinikizo la damu, kiharusi na magonjwa mengine ya moyo.

Mapendekezo

 Ripoti imeweka bayana kwamba hatua za kushughulikia mifumo yote ya utapiamlo kihistoria hua hazijumuishi sababu zikiwemo lishe ya awali kwa watoto, ubora wa lishe, sababu za kiuchumi na kijamii na mazingira ya chakula. Imeongeza kuwa ushhidi unaonyesha kuwa mipango ya kushughulikia lishe duni bila kukusudia imeongeza hatari ya utipwatipwa na ,agonjwa yasiyo ya kuambukiza katikanchi za kipato cha chini na cha wastani ambako mifumo ya chakula inabadilika kwa kasi.

Ripoti imetaja hatua za kuchukua ili kukabiliana na lishe duni na pia utipwatipwa kuwa ni pamoja kuboresha huduma za afya ya mtmama na mtoto, unyonyeshaji maziwa ya mama, mfumowa ustawi wa jamii, na mifumo mipya ya chakula na kilimo  pamoja na sera za lishe bora.

Ripoti inasema kuna fursa ya kutumia nafasi na nyenzo zilizopo kukabiliana na changamoto hizo mbili kubwa na fursa yenyewe ni sasa.

TAGS:WHO, Lancet, utipwatipwa, utapiamlo, afya, lishe duni

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter