Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunahofia sheria mpya ya uraia India , inabagua:OHCHR

Ukumbi wa Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambamo kwalo wataalamu wa haki za binadamu huchangia hoja kuhusu haki za binadamu
UN Photo - Jean-Marc Ferre
Ukumbi wa Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambamo kwalo wataalamu wa haki za binadamu huchangia hoja kuhusu haki za binadamu

Tunahofia sheria mpya ya uraia India , inabagua:OHCHR

Haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR), leo imesema inatiwa hofu na sheria mpya ya uraia iliyofanyiwa marekebisho nchini India kwamba kimsingi ina asili ya unbaguzi. 

 Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi msemaji wa ofisi hiyo Jeremy Laurence amesema “sheria hiyo iliyorekebishwa inataka kuongeza kasi ya mchakto wa uraia kwa makundi ya kidini ya awaliowachahe ikiwataja hususan Wahindu tu, Singasinga, Wabudha, Wajamatini, Waparsis na Wakristo  ambao wakikimbia mateso huko Afghanistan, Bangladesh na Pakistan, ambao wamekuwa wakaazi kabla ya 2014. Lakini haitoi ulinzi huo huo kwa Waislamu, pamoja na madhehebu ya vikundi vingine vichache.”

Ameongeza kuwa sheria hiyo iliyorekebishwa itaonekana kudhoofisha ahadi ya kuhakikisha usawa iliyowekwa hapo kabla katika katiba ya India na majukumu ya India chini ya mkataba wa Kimataifa kuhusu haki za kiraia na kisiasa na mkataba wa kutokomeza ubaguzi wa rangi, ambao India ni nchi mwanachama, mkataba ambao unakataza ubaguzi unaotegemea misingi ya rangi, kabila au dini. 

 Ijapokuwa sheria pana za uraia India zinabaki palepale, marekebisho haya yatakuwa na athari ya kibaguzi kwa wsku kuweza kupata fursa za utaifa.

 Ofisi hiyo imesisitiza kuwa wahamiaji wote, bila kujali hali yao ya uhamiaji, wanastahili heshima, kulindwa na kutimiziwa haki zao za kibinadamu. Miezi 12 tu iliyopita India iliidhinisha mkataba wa kimataifa kuhusu Uhamiaji Salama, wa mpangilio na wa kawaida ambao ambao unayafanya mataifa kushughulikia mahitaji ya wahamiaji walio katika hali ya hatari, kuepuka kuwashikilia kizuizini na kufukuzwa, na kuhakikisha kuwa hatua zote za utawala wa uhamiaji zinazingatia misingi ya haki za binadamu. .

 Wakati lengo la kulinda vikundi vilivyoteswa linakaribishwa, hii inapaswa kufanywa kupitia mfumo wa kitaifa wa uombaji hifadhi  ambao umewekwa kwa misingi ya usawa na sio ubaguzi, na ambao unatumika kwa watu wote wanaohitaji kulindwa kutokana na mateso na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu, bila ubaguzi wa rangi, dini, asili ya kitaifa au sababu zingine zilizopigwa marufuku.

“Tunatambua kwamba sheria hii mpya itatahiminiwa na mahakama kuu ya India na tunatumai kwamba itafikiria kwa makini muingiliano wa sheria hiyo mpya na wajibi wa kimataifa wa India katika utekelezaji wa haki za binadamu.” ameongeza msemaji wa ofisi hiyo ya haki za binadamu.

Wakati huohuo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inatiwa wasiwasi na taarifa kwamba watu wawili wamekufa na wengine wengi wakiwemo polisi kujeruhiwa  katika majimbo ya India ya Assam na Trippura wakati wa maandamano ya watu kupinga sheria hiyo.

“Tunatoa wito kwa mamlaka kuheshimu haki ya watu kukusanyika kwa amani na kuzingatoa sheria, kanuni  na viwango vya kimataifa katika matumizi ya nguvu wanapokabiliana na waandamanaji. Na pande zote zinapaswa kujizuia na machafuko.”

TAGS:OHCHR, India, haki za binadamu, sheria, uraia, Waislam