Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasomali zaidi ya 5000 warejea nyumbani kwa hiari kutoka Yemen:IOM/UNHCR

Miongoni mwa wasomali waliorejea nyumbani kwa hiari kutoka Yemen tangu mwaka 2017 akiwa kwenye boti safarini kurejea  nyumbani
©UNHCR/Marie-Joëlle Jean-Charles
Miongoni mwa wasomali waliorejea nyumbani kwa hiari kutoka Yemen tangu mwaka 2017 akiwa kwenye boti safarini kurejea nyumbani

Wasomali zaidi ya 5000 warejea nyumbani kwa hiari kutoka Yemen:IOM/UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Mashirika ya Umoja waMataifa la uhamiaji IOM na la kuhudumia wakimbizi UNHCR yamesema  yamewasaidia wakimbizi wa Kisomali 5087 kurejea nyumbani kwa hiyari tangu kuanza kwa mchakato mwaka2017.

Katika safari ya karibuni boti iliyobeba wasomali 145 imeondoka leo kwenye bandari ya Aden Yemen na itawasili bandari ya Berbeda Somalia kesho Ijumaa Desemba 13.

Kurejea nyumbani kwa hiyari ni sehemu ya mpango wa UNHCR ambapo wa (ASR) IOM ni mshirika mkubwa na UNHCR inasimamia mpango huo Aden, mji wa Al Mulkalla jimbio la Hadramaut na Kharaz jimbo la Lahj na wakimbizi wa Kisomali wanaweza kwenda kwenye vituo hivyo kupata ushauri nasaha na kuurodhoshwa kwa ajili ya kurejea nyumbani.

UNHCR kwa kushirikianana IOM inawasaidia wakimbizi hao wa Kisomali kwa kuwapa nyaraka, usafiri na msaada wa fedha taslim ili kuwezesha safari zao.

IOM husaidia zaidi upande wa operesheni kama kukodi boti,kutoa msaada wa huduma za afya wanapowasili na usafiri kwa wakimbizi kufika katika sehemu ya mwisho wa safari yao. Mwakilishi wa UNHCR nchini Yemen Martin Manteaw amesema “Mgogoro unaoendelea Yemen umefanya kuwa vugumu kwa wakimbizi wengi kuweza kukidhi mahitaji ya msingiya familia zao na kujikimu hasa ukizingatia fursa finyu walizonazo katika kufanya kazi na ugumu wa kiuchumi. Baadhi ya wakimbizi sasa wanachagua kurejea nyumbani na ni muhimu kwa UNHCR kuendelea kusaidia ambao wanataka kurudi kwa hiyari nyumbani kufanya hivyo kwa usalama na utu.”

Mkimbizi wa kisomali aliyekuwa akiishi Yemen akipanda chomboni katika bandari ya Aden nchini Yemen tayari kurejea nyumbani
©UNHCR/Marie-Joëlle Jean-Charles
Mkimbizi wa kisomali aliyekuwa akiishi Yemen akipanda chomboni katika bandari ya Aden nchini Yemen tayari kurejea nyumbani

Yemen ni muhifadhi mkubwa wa wakimbizi

Yemen inahifadhi kundi kubwa la pili la wakimbizi wa Kisomali duniani ambao bi takriban 250,000. Ni taifa muhifadhi wa wakimbizi kwa miaka mingi katika ghuba ya Arabia na pia imeridhia mkataba wa kimataifa wa wakimbizi na vipengele vyake.

Lakini baada ya zaidi ya miaka minne ya vita nchini Yemen hali kwa raia, wakimbizi, waomba hifadhi na wahamiaji imezorota sana na zaidi ya watu milioni 24 wanahitaji msaada wa kibinadamu katika mgogoro huo mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani.

“Kwa wakimbizi ambao wamechagua kurejea nyumbani kwa hiyari ni muhimu kwamba wasafiri kwa usalama na kuunganishwa tena katika jamii zao za asili na hilo linawezeshwa” amesema mkuu wa operesheni za IOM nchini Yemen Christa Rottensteiner.

Safari 39 za kurejesha wakimbizi kwenda Somalia zimefanyika hadi sasa tangu kuanza kwa mpango huo wa ASR miaka miwili iliyopita ukiendeshwa na UNHCR, IOM kwa ushirikiano na washirika wengine wa masuala ya kibinadamu na mamlaka za Yemen na Somalia.