Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wajibu wangu kuhakikisha namhudumia kila mgonjwa:Dkt Rehman

Mwanamke akichota maji nchini Pakistan
UNDP Pakistan
Mwanamke akichota maji nchini Pakistan

Ni wajibu wangu kuhakikisha namhudumia kila mgonjwa:Dkt Rehman

Wahamiaji na Wakimbizi

Kutana na Dkt. Saleema Rehman mkimbizi kutoka Afghanistan anayekonga nyoyo na kuokoa maisha ya wagonjwa wengi nchini Pakistan, baada ya kuvunja kila mwiko wa utamaduni atokako. 

Ni Dkt mkimbizi Saleema Rehman alivuka kila kihuzi kufikia alipo nchini Pakistan. Katika hospitali hii ya Holly Family jimboni Rawalpindi anafanyakazi kama dakatari wa wazazi na upasuaji.

Kila siku Saleema anazalisha watoto wapato 5 na kuhudumia baadhi ya watu masikini kabisa nchini Pakistan wakiwemo wakimbizi kama yeye,“kwangu mimi kila mgonjwa ni mgonjwa lakini wakiona kwamba mmoja wao yuko hapa, wanajiamini na wanahisi furaha kuniona”.

Kuna wakimbizi zaidi ya milioni 1.4 kutoka Afghanistan  walioko nchini nchini Pakistan lakini hakuna mwanamke ambaye ni daktari isipokuwa Saleema na hii inampa faraja kubwa baba yake mzazi aliyefanya kila juhudi ikiwemo kusaidia elimu yake na kumfikisha Saleema alipo licha ya mila na desturi zinazofanya watoto wengi wa kike kutosoma,“nilidhamiria kumuelimisha mwanangu kwa kila hali awe mvulana au msichana, tumekuwa tukimuita Dkt Saleema tangu alipokuwa na miaka mitatu tulipompeleka shule kwa mara ya kwanza, mafanikio ya mwanangu ni matunda ya maisha yangu”

Lakini siku za Saleema kuwa daktari zinahesabika,“hapa nafanya mafunzo tu, mafunzo yanaruhusiwa na kusoma kunaruhusiwa , endapo serikali ya Pakistan itaturuhusu wakimbizi wa Afghanistan kufanya kazi hapa, tutaweza kuwa msaada mkubwa kwa jamii yetu. Naweza kuwafanyia kazi lakini pia raia wa Pakistan”

Endapo Saleema atafanikiwa kutimiza azma hiyo basi atakuwa hamasa kubwa kwa maelfu ya wasicha wengine wakimbizi.