Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yataka suluhu za asili za mabadiliko ya tabianchi zichagizwe katika mifumo ya chakula

Hulka na utamaduni wa kuhifadhi vyakula vya asili ni muhimu sana katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Hulka na utamaduni wa kuhifadhi vyakula vya asili ni muhimu sana katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

FAO yataka suluhu za asili za mabadiliko ya tabianchi zichagizwe katika mifumo ya chakula

Tabianchi na mazingira

Shirika la chakulana kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema suluhu zaasili za mabadiliko ya tabia nchi ni muhimu sana na lazima zichagizwe katika mifumo ya chakula.

Akizungumzia jukumu kubwa la kilimo katika kutoa suluhu za asili za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwenye tukio maalum la “kuchagiza hatua za suluhu za asili kwa pamoja 2020” kandoni mwa mkutano wa 25 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi COP25 mjini Madrid Hispania hii leo Mkurugenzi Mkuu wa FAO Qu Dongyu amesema ubunifu ikiwemo kujumuisha teknolojia kwa sasa ni kitovu cha maendeleo endelevu ya sekta ya kilimo.

Amezitaja suluhu hizo kuwa zinajumuisha hatua katika masualaya misitu na mifumo mingine kama udongo, maji, mifugo, bahari na mifumo ya chakula pamoja na mazingira ya chakula na watumiaji.

“Tunajiandaa kubadili mfumo wa chakula, ni lazima tuufanyiembadadiliko mnyororo wa uzalishaji chakula, thamani na wa usambazaji, suluhu pekee ni ubunifu” amesema mkuu huyo wa FAO Dongyu huku akisisitiza ushirikiano na wadau wote katika kufanikisha hili.

Katika taarifa yake pia amesisitiza udhibiti endelevu wa maliasili na kulinda bayoanuai kwa ajili ya kufikia mifumo endelevu ya chakula smbayo itasaidia sana kuboresha kilimo na uzalishaji wa chakula.

Ametoa mfano wa mradi uliotangazwa mapema leo kati ya FAO, Ujerumani na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP wa kuzisaidia nchi zinazoendelea kushughulikia mabadiliko ya tabianchi katika sekta zao za kilimo.

Amesisitiza kwamba FAO itaendelea kushirikiana na kwaribu na wadau wote katika mfumo wa Umoja wa Mataifa, nchi, asasi za kiraia, sekta binafsi, wanazuoni na washirika wote muhimu ili kuongeza ufanisi wa suluhu zilizopo na kuhakikisha kwamba sukuhu za asili zinasalia kuwa kitovu kwa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kulinda bayoanuai.