Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Aung San Suu Kyi aitetea Myanmar ICJ dhidi ya madai ya mauaji ya kimbari

Aung San Suu Kyi  mbele ya mahakama ya kimataifa ya haki, ICJ
ICJ/Frank van Beek
Aung San Suu Kyi mbele ya mahakama ya kimataifa ya haki, ICJ

Aung San Suu Kyi aitetea Myanmar ICJ dhidi ya madai ya mauaji ya kimbari

Haki za binadamu

Myanmar haitovumilia ukiukwaji wa haki za binadamu uliotekelezwa katika jimbo la Rakhine na utalifungulia mashitaka jeshi endapo uhalifu wavita umetekelezwa hapo , Aung San Suu Kyi ameiambaia leo mahakama ya kimataifa ya haki ICJ huko The Hague nchini Uholanzi.

Bi. Suu Kyi ameyasema hayo akilitetea taifa lake ambalo linakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa dhidi ya Waislam wa kabila la Rohinya walio wachache yaliyofunguliwa na serikali ya Gambia kwa niaba ya jumuiya ya ushirikiano wa Kiislam OIC.

Endapo uhalifu wa vita umetekelezwa utahukumiwa ndani ya mfumo wetu wa kijeshi wa haki”- Waziri na mkuu wa serikali Myanmar, Aung San Suu Kyi.

Kiongozi huyo mkuu wa serikali ya Myanmar ambaye aliwekwa katika kifungo cha nyumbani kwa zaidi ya miaka 20 , mara kadhaa na uongozi wa kijeshi uliokuwepo wakati huo , hashtakiwi ICJ mahakama ambayo inashughulikia kutatua mivutano baina ya nchi.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ndio yenye wajibu wa kuwashitaki watu binafsi na mwezi Novemba mwaka huu mahakama ya ICC iliidhinisha uchunguzi wake dhidi ya madai hayo ya uhalifu dhidi ya ubinadamu ikiwemo kuwasafirisha watu kwa shuruti uliotekelezwa dhidi ya watu wa kabila la Rohingya  

Katika maelezo yake kwenye siku ya pili ya kusikilizwa kwa kesi hii mbele ya majaji,  Bi. Suu Kyi ameelezea muongo wa mvutano baina ya Warhihingya katika jimbo la Rakhine ambao asilia kubwa ni Waislam na jirani zao ambao ni Wabudha.

Mtoto huyu mwenye umri wa miaka 6 kutoka kabila la warohingya  nchini Myanmar, sasa anaishi kambini Bangladesh. Baba  yake anasema walilazimika kukimbia baada ya askari kuvamia nyumba yao na kumpiga mwanae huyu pindi alipokataa kuwaeleza alipo baba yake.
© UNICEF/Thomas Nybo
Mtoto huyu mwenye umri wa miaka 6 kutoka kabila la warohingya nchini Myanmar, sasa anaishi kambini Bangladesh. Baba yake anasema walilazimika kukimbia baada ya askari kuvamia nyumba yao na kumpiga mwanae huyu pindi alipokataa kuwaeleza alipo baba yake.

Amesema hali ilikuwa mbaya zaidi 25 Agosti 2017 wakati ambapo jeshi la nchi hiyo lijulikanalo kama Tatmadaw lilipofanya msako dhidiya jamii za Rohingya baada ya mashambulizi yaliyosababisha mauaji katika vituo vya polisi na kundi lililojitenga linalojiita jeshi la Arakan.

Na matokeo yake ilikuwa ni kufungasha virago na kuondoka kwa Zaidi ya Warohingya 700,000 na kuingia nchi jirani ya Bangladesh, na wengi wao waliiambia tume ya Umoja wa Mataifa ilitoeteuliwa kuchunguza kwamba wameshuhudia machafuko yaliyowalenga na ukatili wa hali ya juu.

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu umedaiwa kufanyika na aliyekuwa Kamisha mkuu wa haki za binadamu wakati huo aliuelezea kuwa ulikuwa ni wa “kutokomeza kabila la Rohingya”

Uwezekano  wa dhamira ya mauaji ya kimbari:Suu Kyi

Bi. Suu Kyi ameiambia mahakama hiyo ya ICJ kwamba huwezi kufuta kabia kwamba jeshi la Tatmadaw lilitumia nguvu kupita kiasi ,huku pia akisema kwamba “kwa hakika katika maingira yaliyokuwepo , dhamira ya mauaji ya kimbari haiwezi kuwa ndio nia pekee” na maneno hayo pia yalikuwepo kwenye ripoti ya wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa 2019 kuhusu mazingira yaliyosababisha kuondoka kwa wimbi kubwa la Warohingya kutoka Rakhine.

Kwa mujibu wa ripoti ya tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Myanmar jeshi la nchi hiyo lilihusika na mauaji yaliyosambaa nay a mpangilio ya wanawake na wasichana, uchaguzi wa wanawake na wasichana wa umri Fulani kwa ajiliya kuwabaka, mashambulizi dhidi ya wanawake wajawaziti na watoto, ukataji wa viungo na majeraha mengine kwenye viungo vya uzazi, kuwaweka alama katika miili yao kw kuwang’ata na ameno kwenye mashavu, shingoni na kuwajeruhi vibaya waathirika hao kiasi kwamba hawatoweza tena kushiriki tendo la ndoa na waume zao au kubeba ujauzito na kuwaacha wakihofia kwamba hawatoweza tena kupata watoto.

Akifafanua kwamba mfumo wa jeshi la Myanmarunapaswa kuwajibika kuchunguza na kuhukumu madai ya uwezekano wa uhalifu wa vita ulifanywa na maafisa wake kwenye jimbo la Rakhine, Bi . Suu Kyi amejuta kwamba kesi iliyowasilishwa na Gambia dhidi ya nchi yake “haikukamilika na inapotosha piacha halisi katika jimbo la Rahine nchini Myanmar”.

Warohingya katika kambi ya Kutupalong wakisaidia ujenzi kwenye kambi yao huko Bangladesh
WFP/Saikat Mojumder
Warohingya katika kambi ya Kutupalong wakisaidia ujenzi kwenye kambi yao huko Bangladesh

Endapo watakuwa na hatia jeshi la Tatmadaw watahukumiwa Myanmar

Mkuu huyo wa serikali Myanmar amesema endapo uhalifu wa vita umetekelezwa na maafisa wa vikosi vya jeshi la Myanmar “watashitakiwa nakuhukumiwa kupitia mfumo wetu wa kijeshi, kwa mujibu wa katiba ya Myanmar”.

Kwa kuongezea amesema kwamba haitosaidia kwa utulivu wa kisheria wa kimataifa kwamba nchi Tajiri zenye rasilimali ndio zinazojitosheleza na kuweza kuendesha uchunguzi wa ndani na kuhukumu. Pia amesisitiza kwamba ni muhimu kwa ICJ kutathimini hali Rakhine kwa usahihi na uangalifu.

Aung San Suu Kyi mbele ya mahakama ya kimataifa ya haki, ICJ
ICJ/Frank van Beek
Aung San Suu Kyi mbele ya mahakama ya kimataifa ya haki, ICJ

 

Kesi dhidi ya Myanmar yaainishwa bayana

Mashitaka hayo yaliyowasilishwa na Gambia kwa kuungwa mkono na wajumbe 57 kutoka jumuiyaya ushirikiano wa nchi za Kiislam OIC yanadai kwamba nyuma ya pazia la utesaji na ubaguzi wa muda mrefu kuanzia Oktoba 2016 jeshi la Myanmar (Tatmadaw) na vikosi vingine vya ulinzi walianza operesheni ya kulitokomeza kabila la Rohingya msemo unaotumiwa na Myanmar yenyewe dhidi yakundi la Rohingya.

Vitendo vya mauaji ya kimbari vilivyofuatia vilikuwa na dhamira ya kulisambaratisha kundi la Rohingya kabisa au sehemu kwa mujibu wa kesi iliyowasilishwa na Gambia ikifafanua kwamba kulifanyika mauaji ya halaiki, ubakaji na ukatili mwingine wa kingono dhidi ya Rohingya na uteketezaji wa mpangilio wa vijiji kwa moto huku mara nyingi kukiwa na watu ndani ya nyumba zinazoteketea.