Kampeni ya chanjo ya kipindupindu yaanza Coxs’s Bazar Bangladesh kuwalinda watu 635,000:WHO

10 Disemba 2019

Kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya kipindupindu imezinduliwa leo kwenye kambi ya wakimbizi wa Rohingya huko Cox’s Bazar nchini Bangladesh ikilenga kuwalinda watu 635,000 wakimbizi na jamii wenjeji zinazowahifadhi limesema shirikalaafya duniani WHO.

Kameni hiyo ya wiki tatu katika kambi hiyo na maeneo jirani ni ya kuwalinda walio katikahatari ya kupata ugonjwa huo hasa wakati huu ambapo visa vimeongezeka vya watu kuugua magonjwa yatokanayo na maji na kuhara.

WHO inasema tayari chanjo ya matone dhidi ya kipindupindu imeanza kutolewa katika kambi za wakimbizi na itakamilika tarehe 14 mwezi huu ikiwafikia watoto warohingya 139,888 wenye umri wa mwaka mmoja na chini ya miaka 5 na katika jamii zinazohifadhi wakimbizi hao.

WHO inasema kampeni ilianza tarehe 8 Desemba na itakamilika tarehe 31 Desemba kwa lengo la kumfikia kila mtu mwenye umri zaidi yam waka 1 na watu 495,197 wanatarajiwa kupata chanjo hiyo ifikapo mwisho wa mwaka hu una hivyo kufanya jumla ya watu wote wakimbizi na wenyeji watakaopewa chanjo kuwa 635,085.

Kampeni hiyo inayosimamiwa na kuongozwa na wizara ya afya ya Bangladesh na kitengo cha ustawi wa jamii kwa msaada wa WHO, shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na wadau wengine inawalenga hasa wale waliokosa chanjo baadhi au zote za kipidupindu. Kampeni hiyo ikiwemogharama za uendeshaji inafadhiliwa na muungano wa chanjo duniani GAVI.

Mwakilishi wa WHO nchini Bangladesh Dkt. Bardan Jung Rana amesema “tunahitaji  kuilinda jamii hii dhidi ya magonjwa ya kuhara. Licha ya hatua zilizopigwa kuhakikisha fursa ya upatikanaji wa maji salama na usafi, magonjwa haya bado yanaendelea na kuwa suala linalotia hofu. Takriban asilimia 80 ya jamii za wenyeji zinazoishi karibu na makambi hazijalengwa na kampeni za siku za nyuma nab ado ziko katika hatari.”

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter