Mchango wa vijana ni muhimu katika kuhuisha haki za binadamu: UN

10 Disemba 2019

Mchango wa vijana umeelezwa kuwa ni muhimu na wa lazima katika kuhakikisha haki za binadamu zinadumishwa kote duniani. 

Hayo yamesisitiuzwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kuhusu siku ya haki za binadamu inayoadhimishwa leo Desemba 10 kote duniani. Amesema ulimwenguni kote vijana wanadamana na kikubwa ni “kupaza sauti zao katika masuala ya haki za mazingira, haki sawa kwa wanawake na wasichana , kushiriki katika kufanya maazumzi na kutoa maoni yao kwa uhuru. Wanaandamana kwa ajili ya haki yao na mustakabali wa amani, haki na fursa sawa.”

Na amesisitiza kuwa kila mtu ana haki ya kupata haki zote za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni bila kujali wanaishi wapi, kabila, dini, asili yao, jinsia, mwelekeo wa kijinsia, kisiasa au maoni mengine, ulemavu au kipato, au hali yoyote ile.  Na je vijana wanaipigiwa chepuo wanasemaje? Nimezungunka katika jiji la Nairobi Kenya na kuzungumza na baadhi yao

(MAONI YA VIJANA NAIROBI)

Katika Siku hii ya Kimataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemtaka kila mtu awasaidie na kuwalinda vijana ambao wanasimama kidete kwa ajili ya haki za binadamu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter