Muungano mpya wa maendeleo ya utabiri wa hali ya hewa na taarifa wazinduliwa COP25

10 Disemba 2019

Mashirika 12 ya kimataifa yanayotoa msaada katika nchi zinazoendelea leo yamekuja pamoja kwenye mkutano wa 25 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP25 unaofanyika huko Madrid nchini Hispania  na kuzindua ushirika mpya kwa ajili ya kuboresha masuala ya utabiri wa hali ya hewa, maji na huduma za mabadiliko ya tabianchi  au Alliance for Hydromet Development.

Kwa mujibu wa muungano huo mpya lengo ni kuziba pengo lililopo katika utoaji wa tahadhari za mapema na taarifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi ifikapo mwaka 2030.

Wajumbe wa muungano huo wameahidi kwa pamoja kuchukua hatua ambazo zitaboresha uwezo wan chi zinazoendelea kuwasilisha utabiri wa hali ya hewa wenye ubora Zaidi, mifumo imara ya utoaji wa tahadhari za mapema, huduma za maji na za tabianchi. Wamesisitiza kwamba huduma hizi ni muhimu sana na zinahakikisha mnepo katika maendeleo kwa kulinda uhai wa watu, mali na maisha yao.

Wajumbe waanzilishi wa Hydromet ni pamoja na Benki ya Dunia, Benki ya ujenzi na maendeleo ya Ulaya, Benki ya maendeleo ya Asia, kituo cha kimataifa cha mazingira, mfuko wa tabianchi inayolinda mazingira, Benki ya maendeleo ya Kiislam, Mashirikaya Umoja wa Mataifa lile la mpango wamaendeleo UNDP, la mazingira UNEP na shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO.

Pia ushirika huo uko wazi kwa wajumbe kujiunga katika sekta zote za maendeleo ya umma, wahudumu wa masuala ya kibinadamu na taasisi za fedha zinazotoa msaada wa kuimarisha uwezo wan chi zinazoendelea katika Hydromet.

Umuhimu wa muungano wa Hydromet

Akizungumzia umuhimu wa ushirika huo hasa sasa Katibu Mkuu wa WMO Petteri Taalas amesema,  "sayansi iko bayana wastani wa joto duniani umeongezeka kwa nyuzi joto 1.1 tangu kipindi cha kabla ya mapinduzi ya viwanda na kwa nyuzi toto 0.2 ukilinganisha kati yam waka 2011-2015. Malengo ya tabianchi yanazitaka nchi zote kuwezeshwa na tahadahari za mapema na taarifa bora na muhimu za huduma za mabadiliko ya tabianchi. Nchi nyingi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto ya uwezo wa kutoa huduma hizi. Muungano huu mpya ni chombo cha pamoja cha kuongeza msaada wetu kwa wasiojiweza.”

Naye makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa ajili ya maendeleo endelevu Laura Tuck amesisitiza umuhimu wa jukumu la muungano huu akisemaNi vizuri sana kuona rasmi kila mtu anakuja pamoja kupitia muungano huu nakuahidi kuziba pengo baina ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea katika utoaji wa huduma za tahadahari ya mapema kuhusu masuala ya hydromet . Hii itasaidia kuhakikisha tunakwenda na wakati, na ufanisi katika njia za kuzisaidia nchi kujiandaa kwa ajili ya hatari za mabadiliko ya tabianchi na kuwalinda watu."

Muungano huo unajikita katika masuala makuu manne ya kuyatilia mkazo . Mosi ni kuboresha mifumo ya uangalizi naufuatiliaji kwa ajili ya takwimu bora kwa kuimarisha uwezo nan chi kwa ajili ya operesheni endelevu na kusaka mbinu bunifu za kufadhili uanzishaji wa uangalizi na ufuatiliaji.

Pili ni kuimarisha msaada kwa ajili ya kuweka mnepo na kukabiliana kwa kuimarisha uwezo wa nchi wa mipango ya kuhimili tabianchi.

Tatu kuimarisha mifumo ya utoaji tahadhari za mapema  kwa kuboresha udhiditi wa hatari za majanga kwa kuanzisha mifumo ya kitaifa ya thadhari mbalimbali, kugakikisha taarifa sahihi za hatari, uwezo wa kutoa utabiri wa hali ya hewa na maandalizi ya uwezekano wa majanga.

Na nne ni kuinua kiwango cha uwekezaji kwa ajili ya kuwa na mitazamo thabiti na endelevu  ambayo itaenda Zaidi ya miradi binafsi ikiwemo kuimarisha muungano wa Hydromet kitaifa, kikanda na kimataifa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter