Wanawake wapagazi Bukavu washukuru MONUSCO

9 Disemba 2019

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mradi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO wa kuelimisha jamii kuhusu ulinzi wa mtoto na ukatili wa kingono umesaidia kuongeza uelewa wa jamii kuhusu madhara ya vitendo hivyo. 

 

Bi. Kitambwe huyo ni miongoni mwa wanufaika wa mradi huo uliokelezwa na kikosi cha polisi wa Umoja wa Mataifa ndani ya MONUSCO ukilenga takribani wanawake 100 wapagazi.

Mradi umetekelezwa katika mji wa Bukavu jimboni Kivu Kusini ambapo wanawake hao wanabeba mizigo kutoka Bukavu hadi maeneo ya vijijini yaliyoko milimani kama anavyoelezea Bi. Kitambwe.

"Natoa mizigo kutoka kwenye meli na kisha nabeba kichwani natembea barabarani. Kuna wakati wananipokea kidogo, kisha narudi tena mwaloni nabeba mihogo na wananilipa kidogo."

Hata hivyo anasema kuna changamoto

"Ndio kuna tatizo kwa sababu wanawake wanakumbwa na ukatili kila wakati. Unakuwa umechoka tayari umeshachoshwa na kubeba mzigo halafu tena mwanaume anakufuata si ukatili huo. Unafanya na hutaki."​​​​​​​

Mwanamke huyu mpagazi akashukuru Monusco..

"Leo tunafurahi tunashukuru tena, kwa maana kumbe MONUSCO inatujua, haikufanya ubaguzi wa rangi wala wa kabila, ikatusaidia sisi wanawake wadogo wenye tuko na cheo vidogo sana".​​​​​​​

Lakini pia ana ombi..

"Kama mnataka kutubadilisha, mimi basi niwe mchuuzi, tuwaachie wanaume kazi ya upagazi, mimi ni mwanamke, niende kuchuuza niketi pahala pamoja. Mgongo hautachoka tena, hautakatika"​​​​​​​

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter