Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zao la mwanzi muhimili wa nyumba za Warohingya liko njiapanda:UNHCR 

Wakimbizi wa Rohingya kutoka Mynamar ambao sasa wanaishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Cox's Bazar nchini Bangladesh wakiwa wanajindaa kukabili msimu wa mvua kwa kujenga kutumia mianzi.
© UNHCR/Caroline Gluck

Msaada wa Kibinadamu

Mwanzi zao maarufu na muhimili wa ujenzi wa makazi ya Rohingya nchini Bangladesh uko mashakani kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa limesema shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Shirika hilo linasema baada ya hali mbaya ya hewa kuikumba Bangladesh kwa zaidi ya mwaka mmoja malighafi  ya mwanzi ilianza kupotea, lakini kwa sasa asante kwa mradi bunifu UNHCR wa kuhifadhi mianzi kwa kuisafisha na dawa kwani imewezekana kuongeza muda wa kudumu kwa mianzi hiyo mara mbili au mara tatu hali ambayo imesaidia sio tu kuokoa misitu bali maisha ya watu. Yogesh Gyawali ni afisa msaidizi wa UNHCR

“Mianzi inaletwa hapa, inasafishwa, inatoboloewa katikati na inakusanywa hapa na baada ya hapo inapelekwa kwenye matanki ili kuwekewa dawa.”

Kituo cha elimu kwa ajili ya watoto wakimbizi wa Rohingya kilichojengwa kwa Mianzi nchini Bangladesh
Md. Arifuzzaman
Kituo cha elimu kwa ajili ya watoto wakimbizi wa Rohingya kilichojengwa kwa Mianzi nchini Bangladesh

UNHCR ilifungua vituo viwili ndani ya makazi ya wakimbizi ya Katupalong mwezi Desemba 2018 na Januari 2019 ili kuiwekea dawa mianzi. 

Kwa kutumia mbinu iliyoanzishwa na shirika lisilo la kiserikali la BRAC , wafanyakazi wakimbizi katika maeeneo hayo wanaitoboa katikati mianzi hiyo, wanaikata vigingi nje iili kuwezesha kunyonya maji zaidi na wanailoweka kwa siku 12 hadi15 kwenye matanki yaliyo na maji na dawa na matokeo yake ni mianzi ambayo inaweza kukaa muda mrefu zaidi ya mwanzi wa kawaida.

“Lengo ilikuwa ni kuongeza muda wa kudumu kwa mianzi hiyo kwa sababu unajua tena gharama na bajeti, pia athari za kimazingira.”

Lengo la mradi huu wa UNHCR ni kujenga makazi mengi zaidi ya kudumu na salama lakini pia kulinda misitu ya Bangladesh.