Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafanikio ya operesheni za ulinzi wa amani yanategemea mshikamano wa wanachama:Guterres

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mopti, katikati mwa Mali wakati wa operesheni za kijeshi.
MINUSMA/Gema Cortes
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mopti, katikati mwa Mali wakati wa operesheni za kijeshi.

Mafanikio ya operesheni za ulinzi wa amani yanategemea mshikamano wa wanachama:Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mafanikio ya operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa yanategemea mshikamano wa nchi wanachama hasa katika mchango wao na pia kupitisha maamuzi muhimu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Akizungumza hii leo mjini New York Marekani  katika mkutano wa ngazi ya juu utendaji na ufanisi wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “utendaji na ufanisi ni jukumu la pamoja la wote wanaohusika katika ulinzi wa amani. Na jukumu hili linaanza na Baraza la Usalama majukumu yake, na kisha linaendelea kwa sekretariati na kupitia mimi kama katibu mkuu. Na huko Mmashinani vikosi vya Umoja wa Mataifa, polisi, na wafanyakazi raia wote wana jukumu.”

Ameongeza kuwa utendaji pia ni jukumu la nchi wanachama kama wachangiaji wa askari na polisi, serikali za zinazopokea vikosi, wanachama wa Baraza Kuu kama wachangiaji wa kifedha na watoa msaada wa kujenga uwezo.

Tangu kuzinduliwa kwa hatua kwa ajili ya ulinzi wa amani, tumeona maboresho kadhaa ya wazi.

Guterres amesema,  “dhamira yetu ya kwanza ni kuunga mkono michakato ya amani na suluhisho za kisiasa. Kwa mfano, katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, shukrani kwa ushirikiano wetu ulioimarishwa na Jumuiya ya Afrika, MINUSCA ilichangia makubaliano ya amani na vikundi vingi vyenye silaha ni faida inayoonekana ya kisiasa na usalama ambayo sasa inatekelezwa.”

Ameongeza kuwa katika operesheni zote tumeanzisha mifumo mpya na vifaa vya kutathmini utendaji. Hii ni pamoja na tathmini ya kawaida ya kitengo cha jeshi na polisi, mifumo ya tathmini ya hospitali na njia zingine kushughulikia kazi za wafanyikazi.

Kama matokeo, tunashirikiana na nchi wanachama kwa njia iliyo bora zaidi. Katika visa vingine, tumerudisha vikosi vilivyoshindwa kutekeleza vyema majukumu yake; kwa wengine, tumepeleka washauri au timu za mafunzo.

Katibu Mkuu amezishukuru nchi wanachama 103 ambazo zimetia saini mkakati wa hiyari wa kutokomeza unyanyasaji na ukatili wa kingono  na kusema msaada wao unaendelea kuhitajika ili ahadi hizo zitimie kwa vitendo huko mashinani kila siku. Na kwa wale ambao bado hawajatia saini amewaalika kufanya hivyo.

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres baada ya kufika katika kambi ya MONUSCO Goma DRC (31 Agosti 2019)
UN /Martine Perret)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres baada ya kufika katika kambi ya MONUSCO Goma DRC (31 Agosti 2019)

Mafanikio mengine

Guterres amesema tumepunguza pia idadi ya vitengo vinavyokabiliwa na  mapungufu kwenye vifaa muhimu, kutoka vitengo 23 mnamo 2018 hadi 12 leo, lakini hata hivyo 12 vinahitaji kushughulikiwa na kutatuliwa.

Kumekuwa na maendeleo ya kuongeza idadi ya wanawake katika kulinda amani katika viwango vyote, lakini bado ni hatua inayokwenda polepole na hii ni njia kuu ya kuboresha utendaji, kama ilivyoainishwa katika azimio nambari  2436.

Hata hivyo amesema “mafanikio makubwa yalikuwa katika idadi ya maafisa wa jeshi wanawake na waangalizi ambao wameongezeka mara mbili tangu mwaka 2017, hadi kufikia asilimia 14.5. Walinda amani wanawake kwenye doria huboresha ufanisi wa ulinzi wetu kwa raia wote, na haswa kwa wanawake.”

Mathalani amesema nchini Sudani Kusini, polisi wanawake wanaofanya kazi na UNMISS wameboresha jamii, wakati askari wanawake katika mpango wa MINUSCA wameunga mkono juhudi za kushughulikia masuala yanayohisiana na ukatili wa kijinsia.

Pia amesisitiza kuwa kuimarisha utendaji wa kulinda amani ni pamoja na kuboresha usalama na usalama wa walinda amani. Hapa, pia, tumeona kuna maendeleo.

Kikosi cha anga cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Afrika  ya Kati, CAR, MINUSCA
MINUSCA/Hervé Serefio
Kikosi cha anga cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA

 

Changamoto za ulinzi wa amani

Pamoja na mafanikio yaliyopatikana bado kKatibu Mkuu amesema kuna changamoto katika operesheni za ulinzi wa amani ingawa idadi ya vifo kwa sababu ya vitendo vya uhasama dhidi ya wafanyikazi waliovaa sare vilishuka kutoka 58 mnamo 2017 hadi 27 mnamo 2018 na 23 hadi sasa 2019.

Hii haikuwa kwa sababu vikosi vilipunguza nguvu kidogo, ni kwa sababu viliongeza nguvu kuchukua hatua kuwa ikawezekana pia sio tu kuwalinda raia kwa ubora zaidi, lakini pia kupunguza idadi ya majeruhi.

Pia tunafanya operesheni kuwa zenye kuchukua hatua zaidi kwa kuchanganya juhudi za wanajeshi na wafanyakazi walio raia kuzuia na kujibu vitishodhidi ya  raia ikiwemo kuwezesha michakato ya amani ya kisiasa .

Mfano  katika maendeleo ya hivi karibuni katika eneo la Beni kaskazini mashariki mwa DRC, MONUSCO inatumia mchanganyiko wa vikosi vya kijeshi, vikosi sita na raia kuweza kukabiliana na vitisho na kuwalinda raia.

Hata hivyo huko Mashariki mwa Congo mfano maeneo ya Beni tuna kila sababu ya kuwa na wasiwasi mfano mauaji ya raia zaidi ya 100 yaliyofanywa na  Wanajeshi wa ADF baada ya miaka mingi ya vurugu za kutumia silaha, yameibua mfadhaiko unaoeleweka kwa viongozi wa MONUSCO. Mioyo yetu inaumia kwa wale wote ambao wamepoteza wapendwa wao.

MONUSCO yashiriki kurejesha amani huko Lodja, DRC
MONUSCO
MONUSCO yashiriki kurejesha amani huko Lodja, DRC

 

Tukiganga yajayo

Katika kuangalia mbele Katibu Mkuu amesema tunapaswa kuendelea na ari na kuimarisha ushirika kwa ajili ya hatua za pamoja ili kuboresha utendaji katika ulinzi wa amani na kutaja mambo 10 ya kutilia maanani ambayo ni

Mosi ni kufanya juhudi zaidi kusaidia operesheni za ulinzi katika maeneo yenye changamoto zaidi.

Pili amesema ni lazima kujenga uwezo mkubwa katika vikosi vya ulinzi wa amani ili viweze kutekeleza kikamilifu wajibu wake hususan kulinda raia .

Tatu ni tunapaswa kuimarisha intelijensia , kutathimini hali na kuelewa mahitaji na matakwa ya nchi husika na watu wake.

Nne tunahitaji kuendelea hatua zilizopigwa na operesheni mbalimbali katika mwaka uliopita ili kuqweza kujenga na kuimarisha utekelezaji wa será za haki za binadamu.

Tano amesema walinda amani wanwake ni chachu ya mafanikio. Tunawahitaji zaidi, ni lazima kuondoa vikwazo vyote vinavyowazuia wanawake kupelekwa kwenye operesheni za ulinzi wa amani ikiwemo vitu vya msingi kama ukosefu wa vifaa vya ulinzi .

Sita amesema tunaweza kuongeza juhudi zaidi kupunguza vifo na majeruhi kwa walinda amani kwa kuimarisha ulinzi na huduma ya waliokumbwa na kiwewe.

Saba ni lazima kuziba mapengo ya vifaa ikiwemo helkopta, vikosi vya dharura vya kuchukua hatua na kuviwezesha vitengo kama vya uhandisi, usafiri na huduma za afya.

Nane wale ambao wanatekeleza vitendo vya uhalifu na kujihusisha na uvunjaji wa sheria ikiwemo ukatili wa kijinsia na kingono lazima wachukuliwe hatua na kuwajibishwa.

Tisa tunapanga kujenga mtandao kwa kushirikiana na vikosi b anchi zinazochangia polisi ili kuwa na mfumo mzuri wa utendaji, tathimini na uwajibikaji.

Na kumi na mwisho ni kwamba operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa lazima ziweke viwanggo kwa ajili ya udhibiti wa mazingira na uendelevu.

Amesisitiza kwamba suluhu ya kisiasa inapaswa kusalia msitari wa mbele na kitovu cha juhudi zote za kufikia amani endelevu duniani.