Tunatiwa hofu kubwa na matumizi ya vifaa vya mlipuko Syria:OHCHR

Watoto wakitafuta maji katika katika mji ulioharibiwa kwa vita, Aleppo
UN
Watoto wakitafuta maji katika katika mji ulioharibiwa kwa vita, Aleppo

Tunatiwa hofu kubwa na matumizi ya vifaa vya mlipuko Syria:OHCHR

Amani na Usalama

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) imesema licha ya usitishwaji wa mapigano Kaskazini Mashariki mwa Syria, bado inatiwa wasiwasi na mambo mawili yanayoendelea na athari zake za moja kwa moja kwa raia.

Kwanza, imebaini ongezeko la kile kinachoonekana kama matumizi mabaya ya vifaa vya mlipuko, IEDs katika vitongoji vya makazi ya raia na masoko. Mashambulio haya yametekelezwa hasa katika maeneo yaliyoko chini ya udhibiti wa vikosi vya Uturuki na vikundi washirika na, kwa kiwango kidogo katika maeneo yaliyoko chini ya udhibiti wa vikosi vya Kikurdi vilivyo kaskazini na kaskazini-mashariki mwa Syria.

Na katika maeneo yaliyo ndani ya “eneo lisiloruhusiwa mapigano” huko Idlib na sehemu za Aleppo, kumeshuhudiwa kuongezeka kwa oparesheni za kijeshi baada ya kuongezeka kidogo kwa uadui mnamo mwezi Oktoba.

Ofisi hiyo imeongeza kuwa hofu yao kubwa ni kwamba vifaa hivyo vya mlipuko vinatumika katika maeneo yenye idadi kubwa ya wat una matumizi hayo yanaweza kusababisha mashambulizi ya kulengwa ambayo ni ukiukaji mkubwa wa sharia za kimataifa za kibinadamu na unaweza kuwa ni uhalifu wa kivita.

Aprili 3, 2018 nchini Syria, mtoto katika shule ambayo imegeuka kuwa kituo cha uhifadhi katika kijiji cha Zeyarah, kaskazini mwa mji wa Aleppo
UNICEF/UN0207849/Al-Issa
Aprili 3, 2018 nchini Syria, mtoto katika shule ambayo imegeuka kuwa kituo cha uhifadhi katika kijiji cha Zeyarah, kaskazini mwa mji wa Aleppo

Idadai ya mashambulizi

Tangu kusainiwa kwa mkataba wa usitishwaji wa mapigano Oktoba 22 OHCHR imesema imeorodhesha ongezeko kubwa la mashambulizi ya vifaa vya mlipuko ikiwemo magari yaliyosheheni vifaa hivyo kwenye maeneo yenye watu wengi ikiwemo makazi na ndani ya takribani masoko 12 yaliyo na pilika nyingi, vilevile katika maeneo ya biashara mfano Al-Hassakeh, Ar-Raqqa na Aleppo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na ofisi ya haki za binadamu kumekuwa na mashambulizi angalu 49 ya vilipuzi kati ya Oktoba 22 na Desenmba 3 mwaka huu ambapo 43 kati ya mashambulizi hayo yaliorodheshwa katika maeneo yanayodhibitiwa na vikosi vya Uturuki na washirika wake ambao ni makundi yenye silaha.

Matokeo ya mashambulizi hayo ni vifo vya raia takriban 78 vikijumuisha wanaume 53, wanawake 7 na watoto 18, lakini pia kujeruhiwa kwa watu 307. Vifo 72 na majeruhi 258 ni tyametokea katika maeneo yanayotdhibitiwa na vikosi vya Uturuki na makundi yenye silaha washirika wake.

Wiki iliyopita ofisi ya haki za binadamu inasema raia 12 wakiwemo wanaume 8, wanawake 2 na watoto wawili waliuawa na vilipuzi vilivyokuwa kwenye gari kwenye eneo la makazi la Tel Halaf  na siku hiyohiyo watu wengine sita wakiwemo wanaume 4 na watoto wakiume wawili waliuawa baada ya vilipuzi kulipuka kwenye gari katika kituo cha kujaza mafuta  katika makazi ya raia ya al-Sina’a mjini Tel Abyad jimbo la Kaskazini la Ar-Raqqa.

Mtoto mwenye umri wa miaka 9 akiwa na nduguye mwenye umri wa miaka 6 wakisubiri mgao wa maji huko Aleppo,Syria.
UNICEF/Zayat
Mtoto mwenye umri wa miaka 9 akiwa na nduguye mwenye umri wa miaka 6 wakisubiri mgao wa maji huko Aleppo,Syria.

Kuendelea kwa operesheni za kijeshi

Hofu ya pili kwa mujibu wa OHCHR ni kuendelea kwa operesheni za kijeshi katika eneo lisiloruhusiwa mapigano mjini Idlib. Mashambulizi ya anga nay a ardhini yanayofanywa na vikosi vya serikali na washirika wake yameendelea kulikabili eneo linalodhibitiwa na makundi yenye silaha uyasiyo ya kiserikali mjini Idlib na Aleppo na kusababisha vifo na majeruhi kwa raia.

Kwa upande wake makundi yenye silaha hivi karibuni yameonhgesha mashambulizi dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na serikali ikiwemo maeneo ya Kusini mwa Idlib, Kaskazini Hama na mji wa Aleppo.

Tarehe 21 Novemba raia saba waliuawa na wengine 29 kujeruhiwa kutokana na kinachodaiwa kuwa ni mashambulizi ya makundi hayo yenye silaha kwenye makazi ya raia ya Aleppo. Ofisi hiyo ya haki za binadamu imesema “licha ya usitishwaji mapigano machafuko yameendelea kuripotiwa Kaskazini mwa Syria.

Tarehe pili Desemba pekee raia 10 wakiwemo watoto wa kiume 8 waliuawa na wengine 12 kujeruhiwa  wakiwemo wanawake wawili na wavulana 7 kutokana na mashambulizi ya makundi yenye silaha yenye uhusiano na Uturuki karibu na shule kwenye maeneo ya makazi yam ji wa Tel Rif’at Kaskazini mwa Aleppo. Na katika shambulio baya zaidi Idlib raia 10waliuawa desemba 2 baada ya ya shambulio la anga kwenye soko la mji wa Maarat An Numan.

Na siku hiyohiyo mashambulizi kadhaa ya anga yaliripotiwa kwenye jela kuu na kusababisha vifo vya watu watano wakiwemo mama mmoja raia na Watoto wake wawili waliokuwa wakimtembelea ndugu wa familia jela.

Sasa ofisi ya haki za binadamu imetoa rai” Tunazitana nchi kuchukua hatua Madhubuti kukomesha ukiukwaji huu unaofanywa na washirika.Tunazikumbusha pande zote katika mzozo wa Syria kuhusu wajibu wao kimataifa wa kulinda raia na kutimiza wajibu wao chini ya sharia za kimataifa.”